Nandy:Niliongea Kiswahili Kuoyesha Uzalendo,Naongea Kingereza Kupita Maelezo

Kumekuwa na maneno ya kumponda mwanadada Nandy anaefanya vizuri katika nyimbo zake kuwa alishindwa kuongea kiingerza baada ya kuhojiwa kwa lugha hiyo  alipokuwa nchini Nigeria wiki iliyopita ambapo aliweza kufanya shoo katika utoaji wa tuzo za AFRIMA na alibahatika kupata tuzo pia.Nandy mwenyewe ameamua kufunguka na kuwaelezea watu kuwa kitendo chake cha yeye kuongea kiswahili katika utoaji wa tuzo hizo alifanya makusudi na sio kwamba hajui kingerza kama wanavyosema.

Nandy anasema kuwa alifanya hivyo ili kuonyesha uzalendo wa nchi yake, lakini pia alifanya hivyo ili watu waweze kuvutiwa na kuhoji  na kutafuta ni nini alichokiongea. Lakini pia hata yule aliyemuhoji alitumia lugha yake kwanza ndio akaongea na kiingerza kwaio yeye kuongea  kiswahili  haikuwa mbaya  kwa sababu alitaka kukitangaza na kuwafanya watu wake wanaomsapoti  pia waelewe.

download latest music    

Nilihitaji watanzania waliokuwa wananianglia kwa sabau ilikuwa ikionyeshwa afrika nzima.wanielewe zaidi kwaio nilileta uzalendo kwanza.Lakini pia nilitaka lugha yetu isambae zaidi kwa sabau watu waliuliza hivi ameongea nini pale, kwaio ataingia ata-google na atatafuta niliongea nini kuliko ningeongea kiingerza ningeahisisha.-Alifunguka Nandy

Nilitaka kuwashukuru ma-fans wangu wote, na nina amini walielewa kwa sabau nilivyomaliza pale walipiga makofi,na pia hata nilivyoongea kiswahili yule dada pale aliniambi ai want you toi teach me swahili, so nikasema yes kumbe umependa eeh, yes i will. -Aliongeza Nandy.

Wasanii wengi wamekuwa wakitia aibu wanapokwenda katika nchi za ugenini kwa kutaka kuongea kiingereza  wakati mwingine hata kiingerza kinakuwa kigumu kwao kuongea, Nandy anaweza kuwa ni moja ya wasanii walioonyesha mfano mzuri kwa kutaka kutangaza utamaduni wao nje ya nchi kwa kuogea lugha yake ya taifa.

Akiendelea kuongelea experience aliyoipta kutoka katika tuzo hizo anasema kuwa imemfanya kuwa huru na ujasiri kuwa kumbe anapendwa na watu wengi Afrika, lakini pia imemuongezea faida kwasababu amekutana na wasanii mbalimbali na kupanga kufanya nao kolabo, na katika hao wasanii wawili aliowataja ni pamoja na Wizkid na Yemi Alade.

Kumalizia Nandy alisema kwa kujigamba kuwa anaongea kiingerza kupita maelezo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.