Napenda Kupigwa na Mpenzi Wangu- Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie supastaa Wema Sepetu ameacha watu midomo wazi baada ya kutoa Kauli ya kwamba anapenda sana pale mwanaume ambaye yupo naye kimapenzi anampiga.

Wema amedai kuwa anapokuwa Kwenye mahusiano anakuwa anaona raha pale mwanaume wake anapompiga japo kidogo pale anapokosea.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa Wema Sepetu aliyasema hayo hivi karibuni kwenye sherehe ya kuzaliwa ya meneja wake, Neema Ndepanya iliyofanyika nyumbani kwa Wema, Salasala jijini Dar ambapo aliulizwa na gazeti la Ijumaa Wikienda kuhusu aina ya mwanaume anayependa kuwa naye

Napenda mwanaume anipe kipigo kidogo siyo mwanaume mnaishi miaka yote, halafu hata kukupiga kofi kidogo hakupigi”.

Wema ameshawahi kusema aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz aliwahi kumpa kipigo cha nguvu kiasi ya kwamba alimuachia majeraha mwilini.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.