Nay Wa Mitego Aitwa Tena Ndani Ya BASATA

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego amefunguka na kukiri kuitwa tena BASATA kwa ajili ya mazungumzo.

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limempatia Nay wa Mitego barua yenye ukarasa mmoja iliyokuwa ikielezea ajenda ya kukutana naye kuwa ni kujadili mwenendo ya kazi zake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nay wa Mitego amefungukia tetesi za kuitwa siku ya kesho katika ofisi hizo na kusema:

Ni kweli nimepokea barua na nitatekeleza wito. Waliniita Basata na nilipokwenda ndiyo nikapatiwa barua yenye ukurasa mmoja na nilipoifungua ndani kuisoma ndiyo nikakutana na maelezo ya kutakiwa kufika Basata Jumanne (kesho) ambapo tutakaa meza moja na uongozi wa Basata kujadili mwendendo na mstakabali wa kazi zangu za kimu-ziki”.

Nay wa Mitego alikaa kimya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kufungiwa kazi yake na BASATA na kuamua kurudi kwa kuachia Ngoma ya Alisema ambayo nayo imeonekana kuleta utata.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.