Loading...

Nay wa Mitego Atupa Dongo Gizani Kwa Wasanii Wanaopenda Kiki

April 16, 2018 at 16:51
Nay wa Mitego Atupa Dongo Gizani Kwa Wasanii Wanaopenda Kiki

Mwanamuziki Ney wa Mitego ametupia gongo gizani bila kutaja ni nani amemlenga katika maneno yake yaliyokuwa yakimaanisha kuwakaribisha mashabiki zake katika kuungalia na kuusapot wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la amsha popo.

Ney wa mitego ambaye aliandika katika ukurasa wake wa instagram ameno yaliyoanshiria kuwa kuna baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa hawaachi ngoma mpaka wapate kiki kwanza anasema kuwa kwa uapnde wake huwa hasubiri kiki ia  nyimbo yenyewe ndio italeta kiki.

Loading...

no hatuogopagi kiki hata siku 1,ukijua unachokifanya  raha sana.nikiamua kudondosha chuma mi nadondosha tu, wao ndio wanaogopa kiki…huku kwetu sisi hatupeleki siku mbele.’–Aliandika Nay katika ukurasa wake wa instagram.

Ukifuatilia kama wiki moja nyumba kuna wimbo wa diamond na harmonize ulitakiwa kutoka lakini wimbo huo ulishindwa kutoka huku kukiwa hakujatajwa sababu  husika lakini wimbo huo ulitoka hivi karibuni.

Kwa inavyoonekana ni kama Ney wa Mitego amekuwa akiwaponda na kuwasema watu ambao wamekuwa na tabia ya kutangaza kutoka kwa nyimbo kisha nyimbo hizo kushindwa kutokwa kwa kuogopa kutofanya vizuri kutokana na kwamba wanakuwa hawajaitengenezea skendo ya kuifanya kusamba kwa haraka.

Hata hivyo kiki imekuwa ni kama mazoea kwa baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakifanya jambo kubwa la ajabu ili kuongelewa katika mtandao ili wanapotoa nyimbo iweze kusikilizwa sana.

Share

Comments

  1. Hehe

  2. Kweli kabisa

  3. Ushasema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…