Loading...

Ndoa Ya Shishi na Uchebe Yafungwa Kimya Kimya

December 07, 2017 at 06:42
Ndoa Ya Shishi na Uchebe Yafungwa Kimya Kimya

Ile ndoa iliyokwa ikisuburiwa kwa muda mrefu ya msanii wa bongo fleva Shilole na mumuwe uchebe hatimaye imefanikiwa kufungwa baada ya kupata misukosuko  kwa muda kidogo. Ndoa iyo iliyofungwa jana usiku ilifungwa kimya kimya huku ikisemekana kuwa iliudhuriwa na watu kumi na tano tu huku ikisemwa kuwa hakuna hata msanii mmoja aliyehusishwa katika ndoa iyo isipokuwa Babutale  meneja ya msanii Diamond ambae ndiie aliyewakilisha upande wa wazazi wa mwanamke.

Hata hivyo ndoa io imewaacha watu wengi midomo wazi kutokana na muda ndoa iyo ilipofungwa na kufungwa kimya kimya bila kualikwa kwa watu ilhali Shiloleh aliahidi kuwa siku ya ndoa yake  angependa watu wajae na wasitoe mchango wowote.

Loading...

Shilole na Uchebe walianza mapenzi yao kwa muda wa zaidi ya miezi tisa sasa huku Uchebe akitoka kwenye ndoa yake ya kwanza ambayo alimpa talaka mkewe na kuhamia kwa Shilole , hata hivyo wawili walishaanza kutangaza dhumuni la kufunga ndoa iyo kwa muda mrefu na sasa wamefanikisha swala hilo.

Ingawa hivi karibuni zilivuja picha za Shilole na mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda ambazo zilifanya watu waamini kuwa uwezekeno wa ndoa iyo kuwepo nimmodgo lakini hatimaye wawili ho wamefanikiwa kuziba watu midomo na kufanikisha adhma yao.KILA LENYEKHERI KWAO.

Leave a Reply

avatar

in Entertainment

Loading…

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.