Nitapunguza Mauno kwenye Video Ila Sio Kwenyee Show;-Snura

mwanadada snura mushi amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amepunguza kabisa kukatika mauno katika video zake na sio kwa sababau ya BASATA lakini tangu alipoanza kutolewa katika kinyanganyio cha kilimanjaro music awards amejifunza na sasa ameanza kupunguza ukali wa video zake.

Hata hivyo mwana dada huyo amesmea kuwa pamoja na kwamba mauno ya kwenye video yatapungu lakini haitapunguza mauno katika show zake kwa sababu anaamini kuwa watu wanaopatikana kule wanaendana na mambo ya show anayoifanya.

download latest music    

Akiongea na Dida katika mitikisiko ya pwani , Snura anasema kuwa video yake ya nimevurugwa ilikuwa ikifanya vizuri lakini ilikuja kufungiwa na kushindwa kuingia katika tuzo  za Kili , hicho kitu kilimuuma sana.

Tayari mimi sasa hivi nimeshabadilika sana kabla hata ya hayo mambo ya kili video yangu ilikuwa imefungiwa na hata wimbo wangu wa ushaharibu ukitoka watu watajua jinsi gani nimeweza kubadilika , kwenye video sio kwamba hakutakuwa na viuno ila nimepunguza.wimbo unaokuja sijakatika kama kwenye nimevurugwa wakati nafanya kule nilijua ni ubunifu na utundu wangu lakini  kumbe sio kweli na wala sikujua kama nitafungiwa.

ninajua nina mashabiki wengi wanaopenda sana viuno vyangu lakini kwenye show sitakuwa nakatika sana naomba wavumilie tu lakini wale tutakao kuwa tunakutana kwenye show nitakuwa najiachia kama kawaida.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.