Nuh Mziwanda Azidi Kumlilia Binti Yake Adai Mama Yake Anaenda Naye Kwa Wanaume Wengine

Msanii wa Bongo fleva Nuhu Mziwanda kwa mara nyingine ametumia mtandao wa kijamii kueleza majonzi yake kuhusiana na malezi ya binti yake Anya.

Nuhu Mziwanda na Mama wa mtoto wake ajulikanae kama Nawal walioana mapema mwaka huu lakini kwa Bahati mbaya ndoa hiyo haikudumu na hivyo kupelekea kuachana na Nawal kuolewa na mwanaume mwingine. Tangu wameachana wamekuwa wakikwaruzana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malezi ya mtoto huyo huku Nuhu akidai mzazi mwenzie anamkataza kumuona binti yake.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nuhu amefunguka yafuatayo:

Nakumiss sana mwanangu Anya yaani Mungu anajua jinsi gani moyo wangu unaenda mbio nikikukumbuka au ukinijia akilini maana najua ungefurahi uwepo wangu karibu yako, Najua hauhisi Upendo kama uliokuwa unahisi ulipokuwa karibu yangu, ningependa nikukuze katika misingi yangu, sheria zangu na kanuni zangu kama baba ako. mama yako hakutendei haki kabisa na mimi natambua hilo anazunguka na wewe kwenye kumbi za starehe, anasafiri na wewe kwenda kwa wanaume wengine haukustahili haya mwanangu”.

Nuhu aliendelea kunung’unika lakini pia alitoa rai hiyo ili endapo akiwa mkubwa aelewe hakuwa kwenye maisha yake kwa sababu mama yake hakumruhusu.

Naandika hii ibaki kama kumbukumbu ukikua najua utaiona mwanangu maana wanawake wengi hupenda kupandikiza chuki kwa watoto ili wachukie baba zao, nimelia sana juu yako ila sasa namkabidhi Mungu hili suala na ninaamini atakulinda atakupa tabasamu sahihi japo upo mbali na mimi nakupenda Anyaghile wangu”.

Mpaka sasa Nawal hajajibu tuhuma hizi alizotupiwa na mzazi mwenzie. Kea sababu kila hadithi Ina pande mbili hatuwezi sana kutetea upande wa Nuhu bila kusikiliza na upande wa Nawal, lakini mpaka apo maoni yako ni nini?

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.