Ommy Dimpoz: Siruhusiwi Kumuongelea Mama yake na Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amefunguka kuwa hawezi kuzungumzia tena ishu yake inayomhusu mama mzazi wa mwanamuziki mwenzake Diamond Platnumz.

Ommy Dimpoz na Diamond ambao walikuwa marafiki wazuri mwanzoni hadi kushirikishana kwenye kazi zao mbalimbali waliingia kwenye vita kali ya maneno wiki chache zilizopita huku Alikiba naye akiwa katika timbwili hilo ambapo inasemekana kuwa ugomvi huo unatokana na wivu wa kikazi kati ya wasanii hao huku kila mmoja akijaribu kwa namba moja kwa nafasi yake.

download latest music    

Ugomvi huo uliishia kuzua makubwa kwani Ommy dimpoz kumuingiza Mama yake na Diamond kwenye sekeseke hilo kwa kudai kuwa ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama huyo na kumwambia Diamond amuite Baba kitendo ambacho kilimuumiza sana Diamond na kuishia kwenda kumripoti polisi na Ommy kuitwa kwa mahojiano.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka haya kuhusu kesi hiyo;

“Kuhusu ilo swala tulishasema tukiongelea tunakuwa tunarudisha mambo nyuma so hata management imesema bwana hayo mambo usizungumzie tena na wewe ujiulize tangia nimetoka safari mpaka nimerudi nimeshakutana na vyombo vya habari vingapi lakini hujaona nikizungumzia kwani nikiongelea tutaamsha hisia za watu kwaiyo inakuwa haijakaa sawa lakini yaliyopita yamepita”.

Lakini pia Ommy aliongezea:

“Central police nilienda kwa vitu vingine ndo maana polisi walisema kama kuna mtu anataka kujua tulikuitia nini aje atuulize mwenyewe hivyo siwezi kuzungumzia kwani ni vitu vya kisheria kwaiyo na mimi saivi sitaki tena kuvunja sheria, lakini hayo mambo yameshaisha lakini nilichoitiwa bado naenda polisi kuripoti kama kawaida lakini hatuko kubaya sana”.

Ommy Dimpoz anafanya vizuri na wimbo wake wa cheche , pia anafanya vizuri kwenye fiesta zinazoendelea kwa kufanya shoo kali.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.