Pretty Kind- Nimeokoka, Sasa Naimba Nyimbo Za Dini

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind ametangaza rasmi kuachana na Bongo fleva na kugeukia Muziki wa Gospel/ nyimbo za dini.

Pretty Kind amefunguka na kuweka wazi kuwa amefikia uamuzi huo Baada ya kuamua kuachana na mambo ya kidunia na kumrudia Mungu Wake kumaanisha kwamba ameokoka.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Pretty Kind alisema baada ya kumrudia Mungu, ameamua kuachana na muziki wa kidunia na sasa anaandaa nyimbo za Injili ambazo ataziachia hivi karibuni.

Tangu nimeokoka maisha yangu yamekuwa ya furaha mno na nina amani moyoni tofauti na nilivyokuwa naendekeza maisha ya kidunia hivyo ili kudhihirisha furaha aliyonipa Mungu, sasa ninaanza kuimba nyimbo za Injili ili ziwe ushuhuda wa kuwabadili na wengine“.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.