Q-Jay Akanusha Taarifa Za Yeye Kuwa Chizi na Kuokota Makopo

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba miaka ya nyuma Q-Jay ameibuka na kukana vikali taarifa zilizoenea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amerukwa na akili.

Taarifa Hizi zilisambazwa na msanii mwenzake anayejuliaka kama Makamua ambaye aliwaomba Watanzania wamchangie Q- Jay kwa madai ameathirika na madawa ya kulevya kiasi cha kuanza kuokota makopo.

download latest music    

Baada ya kusambaa kwa taarifa hizo Q Jay ameibuka na kuzikana vikali ambapo Kwenye mahojiano aliyofanya kituo kimoja cha habari amefunguka haya:

Habari hizo sio za kweli ila kitu kilichotokea ni kwamba nilipitia changamoto fulani Kwenye maisha lakini sio kwamba nilikuwa Chizi naamini hata wewe mwenyewe unaweza ukaona kuwa Chizi hawezi kuongea kama mimi”.

Lakini pia Q- Jay amelaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kudai taarifa hiyo ilikuzwa kutokana na watu kutumia mitandao ya kijamii vibaya:

Kuna watu Wanatumia mitandao ya kijamii vibaya na kuna watu ambao unakuta hawakupendi ninachotaka Watanzania wajue mimi sio Chizi ninafanya kazi zangu vizuri na nimeamua kurejea kwenye muziki rasmi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.