Ray C Amtumia Ujumbe Mzito Wema Sepetu

Msanii mkonwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameibuka na kumuandikia ujumbe mzito msanii wa Bongo movie Wema Sepetu ambaye amefungiwa kufanya sanaa ya maigizo kwa muda usiojulikana.

Siku chache Wema alijikuta katika upande mbaya wa sheria baada ya kuachia video iliyomuonyesha akipata wakati wa faragha na mpenzi wake baada y ahilo Wema aliomba msamaha lakini aliishia kufungiwa kufanya filamu kwa muda usiojulikana.

download latest music    

 

Baada ya sakata hilo Ray C ameibuka na kumpa ujumbe wa kumpa moyo katika kipindi hiki kigumu anachokuwa anapitia.

Kupitia ukurasa wake wa Instgram, Ray C amesndika;

Nakumbuka 2006 Mange alinipigia Simu akaniambia anakuja nyumbani na mshiriki mmoja atakaeperform wimbo wangu kwenye kipengele cha Vipaji kwenye mashindano ya urembo ya (Miss Indian Ocean)na inabidi tumvalishe kama mimi nikamwambia sawa!walipofika nyumbani Kwangu nilimwangalia wema juu mpaka chini na alivyo mrefu,nikamwambia Mange huyu anashinda Miss Tanzania,nakumbuka alikuwa mwembamba,mrembo na mwenye aibu and I was like Wow!!!!

Anyway kiufupi Nakupenda mpaka leo Wema,Maisha ni Kama milima!wewe bado ni mdogo sana na una nafasi ya kuwa utakacho!pamoja na yanayoendelea sasa bado moyo wangu una imani na wewe kuwa utasimama tena zaidi ya juzi jana na leo na Utakua.Never give up!

Dunia inaweza kukubadilikia kutoka kuwa kipenzi cha watu na kuwa Public enemy number one!Its normal!!!Its ok!ila kumbuka Familia yako ndio kila kitu!Please usihuzunike ukajiona wewe ndo mkosaji dunia nzima maana kila binadamu ana majanga yake ni Mungu tu ndio mkamilifu ingawa sio sababu ya kutufanya kurudia makosa over and over again!

Nakupenda na nina imani na wewe!Nakutakia kila la kheri katika maisha yako na natamani kumuona Wema Mpya.Lots of  love @wemasepetu ”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.