Ray Kigosi- Nisingefanana Na Mwanangu Walimwengu Wangenipa Tabu Sana

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Vincent Kigosi maarufu kama Ray amefunguka na kuweka wazi kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kuwa anafanana copyright na mtoto wake Jayden.

Kabla Ray hajazaa mtoto na Muigizaji mwenzake Chuchu Hansy kulikuwa na tetesi kuwa Msanii huyo Hana uwezo wa kuzaa (Tasa/ Mgumba) kwani alikuwa Kwenye Mahusiano na wanawake wengi lakini hakuwa na mtoto.

download latest music    

Lakini mwaka juzi Ray na mpenzi wake wa siku nyingi Chuchu Hansy walifanikiwa kumkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja na kwa bahati nzuri mtoto huyo ni kipindi kabisa ya Baba yake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ray amefunguka na kusema anamshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kufanana naye kwani vinginevyo walimwengu wangemsumbua kwa maneno ya kejeli.

Walimwengu bwana wanaongea sana. Ingetokea mtoto labda kafuata kwa mama kila kitu halafu kwangu hamna kitu, yangeibuka ya kuibuka hadi ungeshangaa, nashukuru sana Jaden amenifichia maneno kwa kufanana na mimi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.