Ray vanny, Vannesa Watusua Na Dili la Essence Marekani

Wasanii wawili  kutoka katika muziki wa Bongo Fleva waliotajwa  kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la EssenceFestival nchini Marekani, wasanii hao ni Vanessa Mdee na Rayvanny.Tamasha hilo ambalo kila mwaka hufanyika huko New Orleans, Louisiana mwaka huu limepangwa
kufanyika kuanzia July 4 hadi 7 mwaka huu.

Wasanii wengine wa Afrika waliotajwa kutumbuiza ni pamoja na Sauti Sol kutokea Kenya, Davido
kutokea Nigeria pamoja na Nasty C wa Afrika Kusini.Wasanii wengine nje ya Afrika ni pamoja na Miss Elliot, Mary J.Blidge, Nas, H.E.R, Teyana
Taylor, Pharrell Williams na wengine.

download latest music    

Tamasha ya Essence fest lilianzishwa na jarida la Essence mwaka 1995 likiwa na lengo la kuwapa
nguvu wanawake wenye asili ya rangi nyeusi na kusherekea tamaduni na muziki wa watu wenye
asili ya Afrika nchini Marekani.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.