“Sasa Nafanya Muziki Kwaajili ya Wanawake” Country Boy

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya Rooftop production Country Boy amefunguka na kudai kuwa kuanzia hivi sasa ataanza kufanya muziki maalumu kabisa kwa ajili ya wanawake.

Baada ya kupata mafanikio makubwa kupitia ngoma zake Kama ‘turn up’ na ‘Mwaah’, sasa Country Boy anasema kuwa ameamua kubadilisha style ya muziki wake na kuamua kuupa ladha ya anayoamini itawavutia zaidi wanawake.

download latest music    

Country Boy amesema kuwa anaamini akiimba bongo fleva laini atawavutia zaidi wan awake na ile hip hop ngumu nyeusi kuwaachia marapa wengine, anesema anaamini hiyo yote ni kugawana majukumu ili kuwapa vitu vizuri mashabiki.

Country boy pia alifunguka kwa Enews ya EATV na kutoa sababu iliyompelekea mpaka mwaka 2017 alitoa ngoma chache tofauti na alivyozoeleka kipindi cha nyuma:

Kwanza kabisa ninaamini katika kazi nzuri kwani imeshatokea sana natoa kazi Leo kesho naulizwa vipi country mbona kimy? Soo mimi naamini sitoi big G ile ambayo unaweza ukaila alfu ikapungua utamu mapema na piano mziki ni biashara kwaiyo sahivi naingia kufanya sana bongo fleva ile laini ya kuvutia watoto wazuri maana kiukweli kabisa mapenzi ni sehemu kubwa sana ya maisha yetu kiukweli kwaiyo nimeona tuhamie sana upande huu na ile hip hop ngumu nyeusi tuwaachie wengine wafanye”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.