Loading…

Shaidi kesi ya Wema Sepetu aongea

September 12, 2017 at 18:04
Shaidi kesi ya Wema Sepetu aongea

Ikiwa ni muendelezo wa kesi inayomkabili tanzanian sweetheart wema sepetu iliyokuwa inasikilizwa leo tarehe 12 septemba,msanii huyo amefika mahakamani na kusikiliza kesi yake.kesi iyo ambayo bado imekuwa ikionekana kuwa na utata katika kupokea ushahidi leo tena shaidi amefunguka kuhusu kile walichokikuta walipoenda kupekuwa nyumbani kwa msanii huyo.

Shaidi huyo aliyejulikana kwa jina la Inspekta wille ameiambia mahakama ya hakimu mkazi kisutu kuwa walikuta msokoto wa bangi katika kabati la vyombo  nyumbani kwa wema sepetu , shaidi huyo anasema kuwa walipofika nyumbani kwa wema walimkuta mdada wa kazi wa nyumba hiyo, ivyo wakaomba kuonana na mjumbe wa nyumba kumi.’Mjumbe alifika na tukamwambia tunataka kukagua nyumba  iyo ili kutafuta dawa za kulevya’

Loading...

Shaidi huyo aliendelea kwa kusema kuwa walianza kukagua na kwenda jikoni ambapo  walikuta msokoto mmoja  wa bangi juu ya kabati pamoja na  lizra, shaidi huyo anasema kuwa baada ya kumaliza kukagua jikoni walienda chumba cha nguo cjha wema ambapo pia walikuta msokoto mwingine unaozaniwa  pia kuwa ni  msokoto wa bangi.

Shahidi huyo anaongezea pia kuwa hata baada ya kukagua chumba icho waliingia chumba cha wadada wa kazi ambapo huko pia walikuta msokoto mwingine wa bangi amabao unaonekana kuwa ulishatumika ukiwa ndani ya kiberiti, na baada ya hapo walisaini hati ya ukamataji na kumkatama wema kumpeleka kituo cha polisi  lakini muda wote huo wa ukaguzi shahidi anasisitiza kuwa walikuwa sambamba na mdada wa kazi kama ambavyo wema mwenyewe alivyoomba.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo vielelezo husika vilitakiwa kukabidhiwa kwa mahakama na shahidi lakini wakili mtetezi wa upande wa pili alikata   na kudai vielelezo vina mapungufu baadhi, hata ivyo kesi iyo bado inaendelea.

Ikumbukwe kuwa wema ni mmoja wa wasanii ambao walikumbwa na sakata la kukutwa na madawa vya kulevya aina ya bangi nyumbani kwake kipindi vita vya madawa ya kulevya ilipoibuka tanzania, kesi ambayo iliwakumba wasanii wengi ,lakini wengine walishamaliza kesi zao .

Comments

  1. yaani kila chumba walipata msokoto mmoja wa bangi? acheni kutuzingua nyie

  2. Huyu shahidi amedanganya,mimi navuta bangi sana,na sio kawaida kuweka kila sehemu..huu ni uongo mtupu

  3. Mwacheni dada aishi,kuna waheshimiwa wavuta bangi mbona wamjawakamata?

  4. Hii kesi sio ya haki,kuna mtu anatafuta kummaliza sepenga kabisa,kama ulikataliwa move on bwana!

  5. Godbless Mwanga : September 13, 2017 at 10:38 am

    Yaani Mungu anawaona mnavyopanga kumdhalilisha mtoto wa watu maskini,ni huzuni enzi hizi za MJP,Tanzania imekua balaa kuishi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.