Shilole apata majibu kutoka kwa Dayna

Hapo awali kabla ya kuachia wimbo wake mpya Kigori alifunguka kudai kuwa sababu yake ya kukawia kabla kuachia wimbo mpya ni kwa sababu alikuwa amewapa wasanii wa kike muda kufanyap projects ambazo ni kali kushinda zake lakini, hakuna aliyeweza kumfikia.

Hata hivyo msanii Dayna Nyange amezungumza na E-Newz ya EATV ambapo alijibu ripoti ya Shilole kwa kusema;

download latest music    

“Mimi nafikiri yeye ndio anaweza kuwa majibu yote kwamba kwa nini amekuja kuchukua game yake, labda alikuwa kimya kwa muda mrefu akawa anaona bado nafasi yake ipo. Unajua kila mmoja ana riziki yake kwenye hizi kazi usitengemee kwamba Dayna atakuja kufanya kitu fulani nimpoteze mtu fulani, hapana kila mta na riziki yake na kila mja na wakati wake,”

Akaongeza kwa kusema;

“I think ni wakati wake kama alifanya kitu fulani akaona mafanikio yake lakini akaona huku bado kulikuwa na mafanikio yake au anahitaji zaidi, so ana haki ya kufanya, kusema anachuku game ni misamiti tu ya lugha zetu za kisanii,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua