Loading...

“Sijawahi Kuchanwa na Viwembe Kisa Mume Wa Mtu

February 11, 2019 at 09:04
“Sijawahi Kuchanwa na Viwembe Kisa Mume Wa Mtu

Mrembo anayetikisa Mitandao ya kijamii kwa umbo lake matata Jane Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kudhihirisha kuwa hajawahi kuchanwa na viwembe kisa kuiba mume wa mtu.

Siku za nyuma kuna stori zilisambaa kwamba Sanchi aliwahi kuchanwa chanwa na viwembe Baada ya kukamatwa na mume taarifa ambazo Sanchi amethibitisha kuwa ni uongo Baada ya kuanika mwili Wake hadharani ukiwa hauna makovu.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Sanchi alisema tangu azushiwe kuwa alichanwa na viwembe baada ya kufumaniwa na mume wa mtu hivi karibuni, hajawahi kuwadhihirishia watu kuwa hana kovu hata moja kwenye mwili wake bali watu walikuwa wakijifurahisha kwa kuongea.

Wale wote waliokuwa wakidai nimechanwa mwili, sitamaniki, basi waangalie halafu wakiona kama nina kovu lolote, waniambie maana watu wanaweza kukuzushia kitu bila sababu“.

Siku mbili hizi Sanchi ameonekana akiwa anajiachia na mavazi ya kuogelea katika visiwa vya Zanzibar alipoenda na Mpenzi Wake kujiachia.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…