Sikutaka Kuwa Meneja wa Karen, Nilitaka Asimame Mwenyewe;-Gadner

Baba mzazi wa mwanadada Karen (GADNER)  amefunguka na kutoa sababu kwanini amekuwa hajihusishi sana na mswala ya muziki ya mtoto wake ikiwa hata yeye yuko katika maswala ya burudani kwa muda mrefu na ukizingatia kuwa amekuwa na jina kwa muda mrefu hivyo ingeweza kumfanya mtoto wake kuwa maarufu na kukuza jina kwa haraka.

Gadner anasema kuwa hakutaka kumsimamia karen kwa sababu alitaka mtoto wake asimame kwa miguu yake na kujivunia mahangaiko yake na sio kuwa nae kila muda, lakini pia Gadner anasema alitaka karen ajitangaze mwenyewe na wala sio kwa kutumia jina lake yeye .

download latest music    

mara ya kwanza nilishauriana na Ruge Mutahaba  kuhusu karen kwa sababu sikutaka kuwa meneja wake na nilitaka asimame mwenyewe, nilitaka ajitambulishe mwenyewe kwa mashabiki zake na  bila kutumia jina langu  ila ikitokea amelta ngoma yake kwenye radio nitamsapoti lakini kwa sasa anafanya kazi yuko chini ya uongozi unaomsimamia.;- Ameongea Gadnr alipokuwa katika mahojiano ya asubui na Clouds360.

Karen ambae kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa lawama na ule uliotoka hivi karibuni wa washa ni mtoto wa kike wa pekee wa mtangazaji Gadner Habash , mtangazaji maarufu kutoka Clouds media.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.