Sina Tatizo Wala Ugomvi Wowote na Barakah the Prince- Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amefunguka na kukataa kuwepo kwa bifu lolote baina yake na msanii mwenzake Barakah the Prince.

Tetesi za wawili hao kuwepo na bifu zilienea baada ya Barakah kujitoa kwenye Label iliyokuwa inamsimamia ya Rockstar 4000 na baada ya muda mchache Ommy kujiunga, Label hiyo ambayo pia inamsimamia msanii Alikiba. Kutokana  na kitendo hicho cha Barakah kujitoa na muda huo huo Ommy kujiunga kilitafsiliwa na wengi kama walijiona hawataiva kwenye chungu kimoja hivyo mmoja wao akaamua kujitoa kwenye label hiyo.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka yafuatayo;

“Sidhani kama Barakah labda alitoka sababu mimi nimekuja hapana, kwanza naamini mi na Barakah tunafanya miziki tofauti yaani hatuna sehemu yoyote tunayoweza kusema hii inaweza ikatokea mkwaruzano, na tunaheshimiana yule ni mdogo wangu namkubali naamini ni moja ya watu wenye kipaji kukubwa kwa hapa Tanzania na kapambana kutengeneza jina lake”.

Ommy Dimpoz pia aliendelea kufunguka;

“Kilichomfanya aondoke Rockstar siwezi kukizungumzia na siwezi kujua ni nini, nafikiri yeye mwenyewe na label wana majibu sahihi zaidi. Siwezi kusema kama nahisi kuna pengo sababu wakati yeye yuko Rockstar mi sikuwepo kwaiyo wenyewe ndo wanaweza kujibu kama kuna pengo la Barakah au hakuna na pia mahusiano yangu mi na Barakah ni ya siku nyingi kabla hajaenda Rockstar yaani tupo sawa tu hatuna tatizo hata kidogo”‘

Ommy Dimpoz kwa sasa anatamba na nyimbo yake ya Cheche ambayo inashikilia namba moja kwenye stesheni za redio mbalimbali na pia kwenye mtandao wa youtube.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.