Sitegemei kushuka kimuziki-Aslay

Mwanamuziki wa Bongo Fleva  ambae hivi karibuni amekuwa akitoa nyimbo nyingi kwa mfululizo na nyimbo zote kupokelewa vizuri na mashabiki , Aslay amefunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa wala hategemei kabisa kushuka kimuziki kwa sababu anaamini nyimbo zake ni nzuri na anaamini nyimbo zake zinapendwa sana.Aslay ambae hivi karibuni mashabiki walimpachika jina la Chris Brown wa bongo  na majina mengine lukuki amesema kuwa kwa upande wake muziki ameanza tangu akiwa mdogo hivyo amekuwa nao hategemei kuchuja katika kazi hiyo.Pamoja na kuvunjika kwa kundi lao lililokuwa linatikisa sana nje na ndani ya nchi kundi la ya Moto Band bado anasema kuwa hiyo kwake haiwezi kuwa sababu kwani wakati anaanza muziki alianza peke yake.

“Nilianza muziki nikiwa peke yangu  na nilikuwa mdogo kiumri , enzi zile za naenda kwa mama  ila niliweza kufanya vizuri  kwaiyo kuingia kwenye kundi na kutoka  sioni kama nitashindwa kufanya  niendelee na muziki nwangu ” anasema Aslay

download latest music    

Kwa Aslay kuvunjika kwa kundi hakuumaanishi kuwa ndio mwisho wa kazi zake kwa sababu anaona hakuna kilichobadilika kabisa, na anaongezea kwa kusema kuwa “kwa sababu naona ni kama zamani tu,ndio maana nafanya vizuri tu , naachia ngoma kila kukicha na ngoma zangu  kali na zinapendwa , mashabiki hawawezi kuzichoka  kwa sababu mimi ni msanii mzuri najua nini ninachokifanya  na sitegemei kushuka kimuziki.”

aslay ameanza kufanya kazi peke yake baada ya kundi lao lilikuwa likifanya vizuri  kundi hilo lilikuwa likijulikana  na kufanya vizuri katika vibao vyake kama  nitakupwelepweta, Cheza kwa Madoido, Niseme Nisisema na Su waliomshirikisha mwanadada  Ruby, kundi ilo lilikuwa likiundwa na Enock Bella, Maromboso na  Beka Flavour pamoja na Aslay mwenyewe.

Aslay ambae sasa ni baba wa mtoto mmoja anavuma kwa nyimbo mpya kwama Pusha, Baby, Mhudumu, na  Likizo ambazo zote zimetolewa kwa kufuatana na zote zinafanya vizuri katika vituo vya radio na televisheni lakini pia mashabiki wamempokea vizuri katika jukwaa la fiesta tamasha linaloendelea sasa hivi nchini.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.