Snura Akiri Kuwa Uvivu Ulimponza Sana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Snura Mushi amefunguka na kuweka wazi Siri Yake ya utoto na kukiri kuwa alikuwa mvivu sana kiasi cha kusingizia ugonjwa akitumwa.

Snura anajulikana kama Msanii mchapakazi ambaye pia mama wa Watoto wawili ambao ameweka wazi kuwa anawalea Watoto Wake mwenyewe, Lakini ameweka wazi pia ameshawahi kuwa mvivu sana wakati mdogo.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Snura alisema haku­wahi kupenda kutumwatumwa, alikuwa ni mvivu na kila al­ipoagizwa kufanya jambo alizua ugonjwa wa tumbo ili tu asifanye kazi husika.

Uvivu huu acheni tu, sasa hivi nikikumbuka najiona mjinga, nilimsumbua sana bibi yangu kwa kusingizia ugonjwa, kila nikiona sasa natumwa naibua ugonjwa ambao sikuwa nao, bibi alinionea huruma na ku­nitungia jina flani kwani niliumwa kila siku“.

Kwenye mahojiano aliyofanya Hivi karibuni Snura aliangua kilio na kuweka wazi kuwa baba Watoto Wake hamsaidii kabisa kulea Watoto Wake hivyo inampasa kufanya kila kitu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.