Snura Amsifia Mpenzi Wake kwa Kujali Watoto Wake

Msanii wa Bongo Fleva, Snura Mushi amesema kuwa mpenzi wake, Minu Calypto amekuwa akijali sana watoto wake kuliko watu wanavyodhani.

Akizugumza na Clouds FM amesema ni kitu ambacho kimekuwa kikimpa furaha kwenye mahusiano yao.

download latest music    

“Anapenda familia yangu yaani anapenda watoto wangu na watoto wangu wanampenda sana. Tunaweza tukawa tunatoka na mtoto wangu wa mwisho akataka abaki nyumbani na mimi ndiyo nitoke,” amesema.

Snura Mushi na Minu Calypto ni wapenzi ambao pia wanafanya muziki. Wawili hao kwasasa wametoa ngoma yao ya pamoja inayokwenda kwa jina la Shoko.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.