Loading...

Steve Nyerere Amefunguka Kuhusu Tuhuma Za Wema Kuhamia CCM Kisa Kuogopa Kuvunjiwa Nyumba

December 06, 2017 at 15:23
Steve Nyerere Amefunguka Kuhusu Tuhuma Za Wema Kuhamia CCM Kisa Kuogopa Kuvunjiwa Nyumba

Muigizaji na mwanasiasa Steven Nyerere amefunguka kuhusiana na tuhuma zinazomkabili rafiki yake Wema Sepetu kuhusu tuhuma za kuhamia CCM Kisa kuogopa kuvunjiwa nyumba.

Mapema wiki hii Wema alitangaza kuwa anahama Chadema chama alichohamia miezi michache iliyopita baada ya kuhama CCM. Baada ya kukaa Chadema kwa miezi michache Wema alitangaza kuwa ameamua kurudi nyumbani CCM jambo ambalo lilizua mijadala mingi kupita kiasi kwani kuna mengi yalisemwa.

Loading...

Moja Kati ya jambo lililozua gumzo ni kuwa inaemekana kuwa Wema alikubali kirudi CCM kwasababu serikali imetishia kuvunja nyumba yao ya familia lakini pia inasemekana kuwa amehaidiwa kuwa kesi yake inayoendelea kuunguruma mahakamani kufutwa na kama angekataa kurudi CCM basi alitishiwa kwenda jela.

Rafiki wa karibu wa Wema na mwenzake kwenye mambo ya siasa Steven Nyerere amefunguka kuhusu tuhuma hizo za kuvunjiwa nyumba alipofanya mahojiano na Millard Ayo Tv:

Habari hizo sio za kweli na ukitaka kujua kuwa habari hizo sio za kweli utaona kuwa Wema bado ana kesi yake mahakamani hayo ni maneno tu ya mjini ambayo watu wanayaongea ambayo hawakatazwi kuyaongea kwani Watanzania sahivi wanacheza na mitandao wanapoteza muda mwingi na kubuni habari zitakazoleta uchochezi ambao hauna tija kwanza ile nyumba ipo miaka nenda miaka rudi leo hiiiwe hivyo kwa sababu gani mbona kuna watu wamefanya makubwa zaidi ya Wema na hawajavunjiwa Nyumbani zao huyo Wema avunjiwe kwa kubwa lipi alilokosa kwaiyo utaona habari hizi ni za uongi na uchochezi  Wema amerudi mwenyewe CCM ameona jua linavyowaka ameamua kurudi nyumbani ili ajipange”.

 

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
1 Comment authors
RichardEricaWinfreyJudyDorothy Recent comment authors
newest oldest most voted
Dorothy
Guest
Dorothy

He he he bwana acha kumchamba Wema

Judy
Guest
Judy

CCM wanataka kuwanunua watu wote wasiwe na pingamizi

Winfrey
Guest
Winfrey

Ni bora maana walikua wameanza kumkimbiza

Erica
Guest
Erica

Chama cha watu ila mwisho wao utafika siku moja

Richard
Guest
Richard

Haya basi isiwe issue sasa


in Entertainment

Loading…

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.