Steve Nyerere Atangaza Kujivua Uongozi Wa Misiba

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere amefunguka na kutangaza kujivua Rasmi nafasi ya kiongozi wa misiba mbali mbali inayowahusu wasanii wa Bongo movie.

Steve amesema ameamua kujitoa katika nafasi hiyo kutokana na fedheha ambayo amekuwa akiipata kutoka kwa watu kutokana na nafasi hiyo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Steve Nyerere amedai kuwa amekua akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake.

Unajua mimi nina wa­toto, sasa wanapoona ya­nayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo wa­tanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nita­shiriki kama mtu wa kawaida”.

Steve Nyerere amekuwa akirushiwa tuhuma mbali mbali na watu ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa Kula rambi rambi ambapo juzi juzi ndugu wa Agnes Masogange walilalamika kuwa hawa kupokea rambi rambi tangu ichangishwe na Steve.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.