“Hakuna mtu anayeninunulia nguo wala kunipa pesa” Agnes Masogange ataja sababu asizoogopa kuuza mwili wake

Aliyekuwa video vixen mkali kutoka Bongo Agnes Masogange amefunguka kuhusu maisha yake huku akigusia kuwa watanzania wengi wanapenda kumponda bure.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Mwanaspoti mrembo huyu alisema Kuwa hana dhiki ikiwa atafikia kiwango cha kuuza mwili wake ili ajitafutie. Masogange alisema,

Agnes Masogange
Agnes Masogange

“Watu bana!, mimi sina dhiki ya kufikia kuuza mwili wangu eti nipate pesa na kuhusu zile picha kipindi kile nilizopiga hazikuwa za utupu sema basi tu watanzania tunapenda kuzusha sana. Na mtu kuenda Sauzi ndio ameenda kujiuza?,” Masogange aliliambia Gazeti la Mwanaspoti.

Aliongeza kuwa hakuna mtu anayemnunulia mavazi anayovaa wala kumpa pesa ya matumizi yake kwa hivyo hakuna anayeweza kumwambia chochote.

“Mimi nilikuwa na biashara zangu nafanya na wanaosema hivyo hawanisaidii chochote,hakuna mtanzania anayeninunulia nguo,hayupo anayenipa pesa waongee tu. Unajua sisi wadada tuna tabia ya kuoneana wivu akiona unafanya vizuri anaanza kukusemea vitu vya ajabu pembeni,”

Sababu ya kesi ya Masogange kutosikilizwa mwezi huu

Agnes Gerald anayetambulika kama Masogange bado anangoja kusikilizwa kwa kesi yake baada ya kutofika mahakamani Jana, Julai 13, 2017 kama ilivyohutajika.

Kulingana na wakili wa mrembo huyu, inasemekana kuwa hangeweza kufika kutoka na kuumwa kwa mwili. Wakili wake, Reuben Simwanza akizungumza na hakimu aliomba radhi kwa mteja wake.

Agnes Masogange
Agnes Masogange

Hata hivyo wakili wa Serikali, Constantine Kakula, hakufurahishwa na maneno haya huku akikumbusha mahakamani kuwa hapo mbeleni Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, alikuwa amepeana amri ya kuwa kesi hiyo ianze kusikilizwa Jana.

Agnes Masogange

Wakili wa Masogange aliweza kuisihi mahakama kuihairisha kesi kesi hiyo hadi July 25, 2017. Masogange hata hivyo ameshtakiwa kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroine na Oxazepam na Heroine.

Mahakama yatoa amri Agnes Masogange akamatwe tena

Video vixen wa bongo Agnes Gerald amejipata mashakani tena baada ya mahakama kutoa amri akamatwe kwa mara ya pili baada ya kutofika mahakamani kwa mara ya pili kesi.

Agnes ambaye hapo mbeleni alikosa kufika mahakamani wakati kesi yake ilikuwa ikitajwa amerudia kosa hili kwa mara ya pili baada ya kutofika mahakamani alipopangwa kutajiwa kesi yake.

Agnes
Agnes

Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ametoa amri hiyo baada ya Masogange na wakili wake kukosa kuwasili. Kwa kosa hili sasa hivi Agnes Masogange atakamatwa kwa kutofika mahakamani na kutotoa taarifa ya kilichofanya kutofika.

Muigizaji huyu ana mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.