Warembo Wa Bongo Movie Wataja Siri Za Bata Za Dubai

Wasanii wanaosumbua katika tasnia ya Bongo movie warembo Aunty Ezekiel na Halima Yahaya maarufu kama Davina wamefunguka na kuanika Siri ya wao kula bata ndefu nchini Dubai.

Davina ameweka wazi kuwa siri kubwa ya wao kuweza kujihudumia na kula bata ndefu Dubai ni Faida za vikoba ambavyo wamekuwa wakijiwekea akiba kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mtandao wa Global Publishers, Davina  alisema watu wasishtuke sana kwa bata hizo kwani Vikoba vyao vina mpango wa kuwapeleka wanachama wake sehemu mbalimbali duniani hivyo wao bata lao wamekwenda kulila Dubai.

Unajua watu wakituona tunakula bata kama hizi wanakimbilia kudhani tumewezeshwa na wanaume, hapana! Na hii naipigia mstari kwa sababu naujua ukweli, sisi tunawezeshwa na mfuko wetu wa Vikoba ambao una maendeleo makubwa na kwa mwaka huu watu wategemee makubwa kwani tuna filamu ambayo tutaicheza pia”.

Wasanii hao wametaja siri yao hiyo kutokana na tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa kuna pedeshee mmoja ambaye amesimamia kuona warembo hao wanakula maisha.

Davina Aamua Kupita Barabara ya Shiloleh

Mwanadada kutoka tasnia ya bongo movies, Davina amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hivi ni wasanii na wanawake wachache sana wanaoshinda masaluni kwa ajili ya kukaa na kutengeneza kucha kwa sababu wanakuwa na mambo mengi ya kufanya na haina haja ya kuwa na urembo usiokuwa na faida.

Davina ambae kwa sasa amekiri kujiingiza katika swala la ujasiriamali wa muda mrefu kidogo huku akihuska na kupika chakula ambacho wateja wake wakubwa ni wanafunzi kutoka chuo cha UDSM.

Sidhani kama kuna msanii anaewaza sasa hivi kwenda kukaa saluni kwa ajili ya kutengeneza au kuosha kucha zake kama ilivyokuwa huko nyuma, siku hizi mimi na jiko na jiko na mimi tu.

Wasanii wengi wa kike kutoka bongo movies kwa sasa wamekuwa wakijitahidi kutumia majina yao na vipaji walivyonavyo kwa ajili ya kujiingiza katika ujasiriamali na kupata pesa kwa njia nyingine tofauti na uigizaji.

Davina Ataja Sababu Za Kuolewa Baada Ya Ndoa Yake Kuvunjika

Msanii mkongwe wa Bongo movie Halima yahaya maarufu kama Davina amefunguka na kutangaza kuwa ana mpango wa Kuolewa Tena hata baada ya kila kiapo cha kutofanya hivyo.

Davina ambaye aliyewahi kuolewa siku za nyuma na ndoa yake kuvunjika ambapo alisema hatakuja Kuolewa Tena amejikuta akisahau kiapo chake na kutangaza Tena ndoa.

Katika Interview yake aliyofanya na Global Publishers, Davina amesema kuwa ni kweli aliwahi kusema kwamba hana mpango wa kuingia tena kwenye ndoa, lakini kwa kuwa ni binadamu kwa sasa wakati umefika na tayari ana mchumba ambaye anatarajia kuingia naye kwenye ndoa mwakani.

Ikiwa mimi ni binadamu niliyekamilika, siwezi kukaa hivi bila kuolewa tena milele, niliyoyasema mwanzo ni maneno tu, lakini kwa sasa tayari nina mchumba na Mungu akipenda nitaingia tena kwenye ndoa mwaka ujao“.

 

Davina Aweka Wazi Mipango Yake Ya Kuacha Kuigiza

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Halima Yahaya maarufu kwa Jina la usanii kama Davina amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kuacha kuigiza endapo atapata kazi ya kumuingizia.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Amani, Davina amesema kuwa sasa hivi ameanza biashara ya kuuza vitu mbalimbali vya urembo lakini yuko mbioni kuzindua na pafyumu yake.

Yaani biashara zangu zikikaa vizuri tu huwezi amini mambo ya kuigiza naweka kando  kabisa maana hakuna tunachopata kama sura tumeuza sana, kipindi hiki ni cha kutafuta pesa tu”.

Wasanii wengi wa Bongo movie wamekuwa wakilalamikia tasnia hiyo na kudai haina maslahi kwa wasanii wengi kuna ambao wamehamia Kwenye Bongo fleva na wengine kuacha kabisa kuigiza na kutafuta kazi za kawaida.

 

Davina- Baada Ya Kuachika Sana Kwenye Ndoa Nimejifunza Mengi

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Halima Yahaya amefunguka na kudai kuwa pamoja na kwamba ameachiwa sana kwenye ndoa zote alizowahi Kuolewa lakini amejifunza mambo mengi kupitia huko.

Davina amekiri kuwa ni kweli hajawahi kupata bahati ya kukaa na mume kwa muda mrefu lakini amejifunza kuwa mwanamke jasiri na shupa I na kuweza kujua kuwa kujituma na kuweza kuwalea watoto wake mwenyewe.

Kwenye mahojiano  na Amani kwa njia ya simu, Davian alisema Mungu amemjalia kupitia kwenye ndoa mbili lakini hakubahatika kukaa kwa muda mrefu lakini kikubwa ni kwamba ndoa hizo zimemfunza mambo mengi sana ya kujituma ili aweze kuwalea watoto wake vizuri.

Siwezi kujilaumu hata siku moja kwa nini sikai kwenye ndoa zote nilizozipitia bali ninachojua ni kwamba zimenifundisha mambo mengi sana hasa ya kujisimamia mimi kama mimi na kuendesha familia nikiwa kama mwanamke mwenyewe bila mtu mwingine pembeni”.

 

Davina Akumbwa na Kashfa ya Utapeli

Staa wa bongo movie Halima Yahaya maarufu kama Davina amejikuta akiingia katika kashfa nzito ya kutapeli watu baada ya jina lake kutumiwa na watu wasiojulikana kutapeli watu katika mtandao wa facebook.

Davina ansema kuwa hakuna kitu kinamuumiza roho na kumsikitisha kama watu wanaotumia jina lake katika mitandao na kufanya utapeli kwa sababu mwisho wa siku sio kila mtu anaweza kuamini kuwa sio yeye anaefanya hivyo , ila kuna wanaojua kuwa yeye ndio tapeli.

kitendo cha huyo mtu kuwa anatumia jina langu kwa ajili ya kuomba ela kwa watu kimekuwa kikinisikitisha sana, na kimekuwa kikinitia doa sana kwa sababu mimi sijawahi kufanya kitu kama hicho hata mara moja.ninawaomba sana watu wae makini katika hilo kwa sababu huyo tapeli mkubwa anatumia vibaya majina ya mastaa.

Hii sio mara ya kwanza wasanii wamekuwa wakilalamika kuwa watu wengi sana kwa sasa wamekuwa wakitumia majina ya wasanii maaufu kufanya utapeli wa kuwaibia watu na mashabiki wamekuwa wakilalamikakwa sababu wanakuwa wanajua kuwa wanaofanya hivyo ni mastaa wenyewe. Katika swala hili hata Jackline Wolper pia alishawahi kuongelea na kusema kuwa jina lake limekuwa likitumia vibaya na hata namba zake za simu.