Mkali Wenu Atangaza Kumzidi Alikiba Kipaji.

Msanii wa vichekesho nchini.  Mkali wenu amefunguka na kusema kuwa tatizo kubwa  kwake ni kwamba hayuko serious na kufanya muziki lakini ikitokea kuwa anataka kufanya muziki basi  anaweza kumzidi hata msanii Alikiba kwa kipaji.

mkali wenu anasema kuwa ameamua tu kufanya kazi ya kuchekesha lakini ikitokea kaamua kuna wasanii wengi sana anaweza kuwafunika katika muziki.

nikiamua kuwa serious kabisa na kuimba,  basi uwezo wangu ni mkubwa zaidi ya alikiba tena ukizingatia na nyimbo zake za ajabu ajabu ndo haniwezi kabisa.

Lakini pia mkali wenu anasema kuwa alishawahi kumuandikia moja ya wasanii kutoka WCB wimbo wa hodari ulioimbwa na Mbosso.

 

Mkali Wenu Ajitangaza Kuwa Bikra

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini  , mkali wenu amejitangaza kuwa yeye ni bikra na hajawahi kabisa kujihusisha na maswala la mahusiano wala tendo la ndo aktika maisha yake yote.Mkali wenu anasema kuwa ingawa watu wengi hawatambui na wala hawataamini hilo lakini ukweli uatabaki kuwa pale pale kuwa yeye yuko hivyo kwa muda mrefu.

Mkali wenu anasema kuwa so kwamba amekuwa na matatizo yoyote lakini amekuwa akipata hisia ambazo  humfanya kutamani kufanya tendo la ndoa lkini amekuwa akijizuia kwa sababu anataka kuja kujisifia na kuiambia familia yake kuwa hata yeye alijitunza sana kwa ajili ya familia yake pia.

Mkali wenu anasemakuwa swal kubwa lilomfanya mpaka kuwa hivyo ni baada ya wanawake wengi sana kuwa wanamkataa huko nyuma na ndio maana aliamua kukata tamaa.

 

 

Harmorapa Amezaliwa kwa Sababu ya Kiki:-Mkali Wenu

Msanii Vichekesho nchini mkali wenu amefunguka na kusema kuwa msanii Harmorapa sio mwanamuziki  bali yupo kwa ajili ya kiki tu na sio kitu kingine.

Mkali wenu anaongezea na kusema kuwa Harmorapa anakuwa hasikiki kwa sababu hana kitu cha kufanya kwa sasa ambacho kinaweza kumpa kiki na ndio maana sasa hivi haonekani katika mitandao.

Harmorapa hakuwa msanii na kujulikana kwa sababu ya muziki,ila harmorapa amejulikana kwa sababu ya kiki, amezaliwa kwa sababu ya kiki tu.harmorapa sio mwanamuziki mzuri yupo kwa sababu ya kiki na kwa sababu hafanyi kiki basi haonekani.

Ninaweza Kuimba Kuliko Alikiba, Diamond:-Mkali Wenu

mwanamaigizo ya vichekesho nchini, Mkali Wenu amefunguka na kusema kuwa ana kipaji kikubwa cha kuimba kuliko hata wasanii wakubwa wanaojulikana sana na wenye majina lakini hajaamua tu kuimba kwa umakini la akiamua  anaweza kufanya zaidi ya hiyo.

Akiongea na bongo5 mkali wenu amabe hivi karibuni ametoa wimbo akiwa amemshirikisha Harmorapa anasema kuwa yeye ni zaidi ya Alikiba, ni zaidi ya Diamond Platinumz au Haromize, mkali wenu anasema kuwa kwa sasa hafanyi muziki kama kitu serious lakini akiamua kufanya kwa umakini basia anweza kufanya vizuri zaidi ya hapo.

Mimi sijaamua tu ngoma yangu iendee sana lakini mimi nakuhakikishia kuwa napenda sana kuimba, na mimi  ninaimba kuliko hata diamond Platinumz, au harmonize, kuliko hata alikba, yule  wa yaah seduce mee..ila sema tu sijaamua kufanya lakini nikaona bora nifanye kitu kidogo tu nikatunga nyimbo, nikaandika na kisha nikamweka harmorapa pale  , kwaio nikiamua kufanya mimi nafanya dadake:- aliongea mkali wenu alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari wa bongo 5