“Ruge Alinisaidia Nilikuwa Mwizi Akanirudisha Kwenye Mstari”- Msami

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Dansa maarufu Tanzania Msami Baby amefunguka na kuweka wazi Jinsi Marehemu Ruge Mutahaba alivyomsaidia na kumtoa kwenye maisha ya wizi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Msami alisema kipindi hicho alikuwa akiishi maisha ya kihuni Temeke ambapo alikuwa mwizi wa kutupwa na tena wa kuvunja nyumba za watu, kuiba mali na kwenda kuuza lakini anamshukuru sana Ruge ndiyo ameweza kuona kipaji chake na kumwambia aachane na hivyo vitu aimbe.

Nitalia siku zote juu ya Ruge, ameniepusha na kifo mimi maana jamaa niliyekuwa naiba naye majumbani kwa watu amesh-auawa. Baada ya Ruge kuniona na kunichukua nilisafiri kwenda Afrika Kusini na niliporudi nilikuta yule rafiki yangu kauawa kwa sababu ya wizI”.

Lakini pia Msami ameweka wazi kuwa moja ya mafanikio makubwa aliyokuwa nayo ni Ruge kumuamini kuwa msanii na kiongozi wa madansa na pia kumfanikishia kununua gari aina ya Toyota IST (nyeusi) ambayo imekuwa ikim-saidia katika kazi zake za kimuziki.

Irene Uwoya ni Mzuri Lakini Huyo Dogo Janja Simjui- Msami

Maanamuziki wa Bongo fleva na Dansa maarufu Bongo Msami Baby amezidi kutengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuendelea  kupostiana na Ex wake Irene Uwoya.

Uwoya na Msami wameendelea kuwaacha watu midomo wazi baada ya kuendelea kupostiana Kwenye mitandao ya kijamii na kusifiana ilihali Ikiwa ni wazi kabisa kuwa Uwoya ni mke wa staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Ishu hii imeleta tafsiri tofauti kabisa hasa ukizingatia kuwa Uwoya ni mke wa mtu na hivyo kusababisha ndoa ya Uwoya na Dogo Janja kukosa heshima mbele ya Jamii.

 

Msami amefanya Interview na Enews ya EATV na kudai haoni kama ni kosa yeye kumsifia Ex wake na kumkubali kama ni mzuri kwani ni ukweli mtupu na haoni kama kamvunjia heshima:

Irene kaniposti kwa sababu anapenda ninachokifanya na ananikibali kwa nini asiseme na mimi kumuandika kama yeye mzuri kwani ni dhambi? sio dhambi kumwambia mtu yeye ni mzuri kwangu mimi binafsi naona kama ni upendo Alafu isitoshe mimi Namjua Yeye huyo mtu wake mwingine mimi simjui mimi najuana na Uwoya tu kwaiyo tuna maisha yetu na stori zetu ambazo tunaongea”.

Msami amesisitiza kuwa hawezi kuacha kuongea na Irene au kumsifia kisa tu ameolewa na haoni kama ameandika kitu kibaya.

Msami Amefungukia Bifu Lake na Irene Uwoya

Dancer na msanii maarufu Msami Baby amefunguka na kuongelea sakata linaloendelea kutengeneza headlines hivi sasa kati yake na staa wa Bongo movie Irene Uwoya.

Msami na Irene Uwoya walishawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma lakini walikuja kuachana na Uwoya amemshirikisha kufunga ndoa na staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Uwoya na Msami walirudi kwenye headlines za mitandao ya kijamii siku ya juzi baada ya Uwoya kuposti maneno yenye utata na kisha Msami naye kumjibu kwa kejeli kuhusu ndoa yake jambo lililozua maneno na watu kufikiri labda wana bifu.

Msami ameongelea suala hilo Kwenye Interview aliyofanya na Soudy Brown kwenye You heard ya XXL:

Mbona mimi sijaona kibaya pale alichoposti Irene mimi naona kama kanisifia kuwa The best dancer in Africa ? Mbona mimi naona kama hajanipaka yaani hajanidhihaki”.

Msami amesema hajui kuhusu ndoa yake hata kama ameolewa lakini hajawahi kumwambia kuwa ameolewa na hata wakikutana hawaongei kuhusu ndoa yake na kuhusu kumposti amesema labda Irene anamiss maudambwi dambwi yake.

 

Simjui Brown, Ila Wolper Akinitaka Namkubali -Msami Baby

Mwanamuziki na dancer Msami baby kutoka nyumba ya vipaji THT amefunguka na kudai kuwa Jacqueline Wolper ni msichana mzuri hivyo akimtaka hawezi kukataa.

Msami ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa bongo movie Irene Uwoya baada ya tetesi kuenea kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Wolper.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5, Msami amedai kuwa hamfahamu mpenzi mpya wa wolper anayejulikana kwa jina la Brown hivo ikitokea Wolpee akamtongoza basi hatasita kuwa naye.

“Mi namjua Wolper simfahamu huyo Brown, mpenzi wa mwisho wa Wolper ninayemfahamu ni Harmonize kwaiyo Wolper ni msichana mzuri akiniambia ananipenda why not bwana?  Alafu sina haja ya kumtumia DM yaani mi namfuata moja kwa moja si ninajua kama anapatikana na yeye kama ananipenda ataniambia basi tutakua pamoja”.

Katika upande mwingine Msami aliweka wazi uhusiano wake na mwanamuziki Nandy;

“Sina uhusiano wa kimapenzi na Nandy, yule ni kama dada yangu au mdogo wangu inawezekana siku moja tukaqa zaidi lakini kwa sasa ni marafiki yaani kwa maana wote tumetokea kwenye familia ya THT kwa hiyo ni kama familia yangu”.

Msami amewahi kukiri kuwa anavutiwa na wanawake wakubwa kiumri kuliko yeye na moja ya mpenzi wake aliyemzidi umri ni mwana dada Irene Uwoya.