Nitapungua Kifua, Miguu Lakini Tumbo No :-Msechu

Msanii peter msechu amefunguka na kusema kuwa amekuwa akikwazwa sana na watu wanaomsema vibaya kuhusu mwili wake hasa upande wa tumbo kuwa amekuwa na tumbo kubwa limemzidia na hataki kulipunguza.

Akiongea na moja ya waandishi, Peter Msechu anasema kuwa watu wamekuwa wakimuona akiingia gym na kudhani kuwa anateseka sana  na tumbo alilonalo lakini kitu wanatakiwa kujua ni kwamba kamwe hatokaa aangalie namna ya kuondoa tumbo kwa sababu kuondoa tumbo ni mateso na wala hafikirii kulipunguza.

Peter anasema kuwa , Nitapunguza kila kitu lakini sitapunguza tumbo, nitapunguza tumbo, kichwa a kila kitu lakini tumbo nalitamani pale pale.Tumbo huwa ni rahisi sana kuliongeza lakini sio kulipunguza , mimi napenda sana wali maharage na linazidi kurefuka lakini sijashindwa kulipunguza.

Peter Msechu Amerogwa Kigoma :-Baba Levo

Msanii wa muziki wa Bongofleva na Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma, Crayton Chipando (Baba Levo), amesema kitambi cha Peter Msechu kinatokana na kurogwa.Baba Levo amedai Peter Msechu amerogwa kwa kuwekewa ujauzito baada ya kumtia mimba mtoto wa mzee mmoja huko mkoani Kigoma.
Akiongea kupitia eNEWZ Baba Levo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho baba wa msichana huyo alikasirika baada ya Peter Msechu kumuacha msichana huyo hivyo akaamua kuhamisha ujauzito wa binti yake na kumuwekea msanii huyo.

Baba levo aliendelea kusisitiza kwamba “Peter Msechu aachane na ‘GYM’ kwasababu ile ni mimba ambayo amepandikizwa na mzee mmoja kutoka Kigoma na Januari atazaa endapo tu hatakwenda kuomba msamaha kwa baba wa binti huyo”.

Baba Levo alimalizia kwa kusema kwamba Peter Msechu hapaswi kujifananisha na yeye kwa kuwa yeye ni diwani ambaye amechaguliwa kwa kura za wananchi na ni lazima ale vizuri kwa kuwa wananchi wanamtegemea yeye ili kuweza kuwaletea maendeleo katika kata ya

Peter Msechu Afunguka Jinsi Alivyonusurika Kifo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Peter Msechu amefunguka na kuweka wazi jinsi alivyo nusurika kufa kutokana na uzito mkubwa uliokuwa umemuelemea.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, baada ya kuulizwa juu ya kupotea kwake kwenye gemu kwa kupunguza vurugu za kuachia kazi kama ilivyokuwa mwanzo, Msechu alisema yupo ‘busy’ anahudumia kwanza afya yake.

Ni kweli nipo kimya kwa maana kwenye gemu kwa sasa ninanusa nusa tu tofauti na ilivyokuwa zamani. Nafanya hivi kwa sababu sasa ninahudumia afya yangu.

Unajua nilikuwa nimejiachia sana kiasi kwamba nikawa nimefikisha uzito wa kilo 184 jambo ambalo lilikuwa ni hatari sana kwangu”.

Msechu alidai baada ya kufikisha uzito huo mkubwa alijikuta katika wakati mgumu kwani kuna kazi ambazo alikuwa hawezi kuzifanya tena:

Niliamua kwenda hospitali kwa ajili ya kufanya vipimo. Baada ya kufanyiwa uchunguzi niliambiwa tatizo ni uzito maana nina kilo nyingi pamoja na mafuta ambayo ilikuwa imefika hatua yamezunguka moyo.

Nikaambiwa kwa hali ilivyokuwa inakwenda, muda wowote ningezimika tu ghafla kama nisipochukua jitihada za dhati za kupunguza mafuta”.

Msechu amedai tangu hapo kutokana na maelekezo ya daktari ameweza kukata jumla ya kilo zaidi ya ishirini.

Peter Msechu Akana Tetesi Za Kufulia Kimuziki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na ngoma zake kama vile Relax na Nyota amekataa tetesi ambazo zineku a zikisemwa juu yake kuwa amefulia.

Tetesi za Peter Msechu kufulia zilitokana na ukimya wake Kwenye gemu kwa kipindi kirefu bila ya kuwa na nyimbo iliyofanya vizuri kwa muda mrefu kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Peter Msechu amesema kwa sasa anaimarisha shughuli zake za ujasiriamali ambazo zinamuingizia kipato kikubwa cha kuandaa sherehe, kupamba maharusi na shughuli mbalimbali za kijamii.

Ninawezaje kufulia kimuziki? Kwa watu wanaonifuatilia wataona pia nimefanya kava ya Wimbo wa Sitabaki Nilivyo. Hiyo inaonyesha kwamba bado nipo na uwezo wangu ni mkubwa. Ila nimeamua kidogo kuimarisha kwanza masuala yangu ya ujasiriamali tu“.

Peter Msechu ameweka wazi kuwa kwa sasa anafanya muziki jitihada zake amezielekeza Kwenye biashara zake zitakazoweza kumuingizia kipato kikubwa kitakachoweza kumkwamua kimaisha.

Peter Msechu Adaiwa Kuachwa na Mchumba Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Peter Msechu aliyetamba na wimbo wake wa ‘ Nyota’ na Malava amekumbwa na kashfa nzito ya kuachwa na mchumba wake na mama wa watoto wake.

Kwa habari za kimbea zilizo chini ya kapeti zimedai kuwa mwanamke huyo ambaye Peter Msechu amekuwa naye kwa miaka mingi na kumvalisha pete ya uchumba miaka mitatu iliyopita amemuacha huku sababu zikipingana kwani kuna waliodai ameachwa kwa sababu ya uzito mkubwa na wengine wanadai chanzo ni wadhfa.

Baada ya tetesi kutembea kwa muda kidogo Peter Msechu amefungukia tuhuma hizo kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL ya Clouds Fm ambapo amesema haya;

Hayo ni mambo yangu binafsi ya kifamilia yaachwe yamalizike kifamilia mengi yanasemwa sana lakini mimi mwenyewe nitasema muda muafaka ukifika na pia naomba watu wasitunge tu vitu vyao wasubiri wasikie tamko kutoka kwa muhusika ambaye ni mimi ila familia yangu ipo Salama kabisa kama kuna la kusema basi nitasema ila kwa sasa tuache tu na mimi namuachia Mungu”.

 

Mke Wangu Nimemvisha Pete Huu Mwaka Wa 3 Hakuna Harusi – Peter Msechu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Peter Msechu aliyetamba na ngoma zake kama Nyota na nyinginezo amefunguka na kueleza kuwa mwanamke anayeishi naye na aliyezaa naye mtoto hajafunga naye ndoa mpaka leo.

Msechu alifunguka na kuongelea hayo baada ya harusi ya staa Shile na mume wake Uchebe kuzizima na kuvutia wengi ikiwemo mastaa wenyewe. Ndoa hiyo iliyokuwa imehudhuriwa na mastaa kibao ilifana kupita kiasi huku mastaa hao wakiacha rekodi baada ya kumwaga mizawadi kibao kwa maharusi.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo TV Peter Msechu amefunguka Mengi kuhusu kuvutiwa na harusi hiyo na mipango yakea ya kufanya harusi yake mwenyewe:

kwanza ningependa kumpongeza Shilole na bwana Uchebe kwa kufikia maamuzi makubwa ya namna hiyo unajua sisi wasanii ambao tumeshakaa na familia zetu kwa muda mrefu kufanikisha hatua hiyo bado kwa kweli wanahitaji kupongzwa mimi binafsi nilishataka kufunga harusi muda mrefu sana lakini kila nikitaka kuanza kufunga harusi bikifikiria kianza vikao haaa naachia kati yaani ninavyokwaambia mwanamke wangu nimemvisha Pete huunimwaka wa tatu kila nikitaka ya mipango nikiwaza hela ya harusi nakumbuka ndani unga Hamna”.

Baada ya ndoa ya Shilole na Uchene mastaa kibao wamesema na wenyewe wako nyuma wanafuatia mastaa kama Dogo Janja na Irene Uwoya.