Petit Man Athibitisha Kuwa Hana Bifu na Familia Ya Esma

Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache amefunguka na kuweka wazi kuwa hana Bifu na familia ya aliyekuwa mke wake Esma Platnumz.

Petit amesema kuwa hata Baada ya kuachana na Esma Platnumz amekuwa hana tatizo na familia yake na ndio mama yeye na mkwe wake Mama Diamond bado wanaongea vizuri bila tatizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mtandao wa Dizzim Online, Petit Man amefunguka haya:

Sina ugomvi wowote na familia ile, ndio maana hadi leo unaona mimi na mama tunaongea vizuri tunakomentiana vizuri kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi“.

Petit Man na Esma waliachana miezi michache iliyopita Baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka minne na kuzaa Mtoto mmoja pamoja.

Karen-Sijapata Mwanaume Wa Kuwa Naye Kwenye Mahusiano

Msanii mchanga kabisa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Washa’ Karen Gadner Habash amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpenzi kwa sababu hajapata mwanaume wa kuwa naye.

Karen alitengeneza headlines wiki chache zilizopita baada ya kusemekana kuwa kwenye mahusiano an kufunga ndoa na mume wa zamani wa Esma Platnumz, Petit Man Wakuache.

Karen amefunguka kuwa hana mahusiano na Petit Man kama ambavyo wengi walidhani bali ni marafiki tu na ni mtu ambaye aliamua kumsapoti kwenye kazi yake baada ya kuona wimbo ulihitaji kuwa na wanandoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Karen ameweka wazi kuwa hana mpenzi kwa sasa lakini endapo atatokea na katika muda sahihi basi atakuwa hana neno;

Kusema ukweli sina mpenzi kwa sasa nipo single lakini kama atajitokeza na kwa mtu ambaye nitakuwa namuhitaji basi nataka awe muelewa kuhusu kaiz yangu nzima ya usanii na aweze kunisapoti sana lakini pia aipende sana familia yangu hasa wazazi wangu kikubwa aweze kuwaheshimu”.

 

Karen Gadner Afungukia Ndoa Yake na Petit Man

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Karen Gadner amefungukia tetesi zilizomzunguka hivi sasa kwa kuwa amefunga ndoa na mdau wa muziki wa Bongo fleva Petit Man.

Tetesi za Petit kuwa na Mahusiano na Karen zilianza kupamba moto Wiki chache zilizopita baada ya kuonekana kama wanavaliana nguo lakini sakata hilo limechukua Sura mpya baada ya Tetesi za ndoa.

Picha zinazoonekana Kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kama wawili hao wamefunga ndoa lakini kuna taarifa kuwa inawezekana ikawa sio ndoa bali ni video ya wimbo mpya wa Karen wanashoot.

Baada ya sintofahamu Hizi mtandao wa Bongo 5, ulimtafuta Karen na kutaka kumuhoji kuhusiana na tetesi hizo za ndoa na Petit.

Picha nilizoweka zinajielezea tayari kwa kile kilichotokea, kwa sasa siwezi kusema kitu kingine nimechoka Jamani”.

Karen alikataa kufunguka kwa undani zaidi kuhusu kilichotokea na kuwataka watu waendelee kisubiri kwani watajionea mwishoni.

Petit Adaiwa Kufunda Ndoa ,Mwanamke Wake Bado ni Kitendawili.

Wikiendi yote imepita lakini habari zinazosambaa katika mitandao ya kijamii ni kuhusu ndoa ya Petit man na mwanamke asiejulikana kama kweli ndio huyo anaesema katika mitandao ya kijamii au la.

Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa petit amekua na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada careen ambae ni chipukizi katika muziki wa bongo , mwanadada ambae pia anaweza kuwa na umaarufu kutokana na kazi nzuri anayofanya baba yake Gadner G Habash.

Hata hivyo Petit mwenyewe alithibitsja kuwekpo kwa tukio la kufunga ndao ingawa badi haijaafahamika kuwa ndoa hiyo amefunga na mwanamke gani.

Hata hivyo kurasa nyingi za uadaku zimkeuwa zikimtangaza Careen kama mke mpya wa Petit huku wakimpa mapovu mengi mke wa kwanza wa petit ambae ni dada wa msanii Diamond Planumz anaejulikana kama Esma Platinumz.

Petit Afunguka Mahusiano Yake ya Kimapenzi na Mtoto wa Gadner

Meneja wa wasanii mbalimbali amefunguka na kukanusha madai mbalimbali yanayoedelea katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye kuwa na mahusiano na mtoto wa mtangzaji maarufu Gadner G Habash.

Gadner amekanusha hayo na kusema kuwa pamoja na kwamba yeye na Kareen wamekuwa marafii kwa muda mrefu na kuwa amekuwa akimchukulia kama mdogo wake , na hakuna mahusiano yoyote ya kimapenzi yanayoendelea kati yao kama watu wanavyosema.

watu wanaongea sana kuhusu Careen wanashindwa kuelewa kuwa mimi na careen ni marafiki tu na  kwamba nina mchukulia kama mdogo wangu na rafiki yang tu.Lakini watu wana midomo kwaio lazima waseme

Petit Man Ajibu Kuhusu Kibendi cha Mnyarwanda.

Moja ya watu maarufu katuka tasnia ya bongo Petit Man ambae pia ni mume wa mwanadada Esma platinumz ambae ni dada wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake kama kweli kuna mwanamke ana ujauzito wake hana shida azae tu yeye hakatai mtoto.

Petit man anasema kuwa mtoto kwake ni baraka ukizingatia yeye hana watoto wengi bali ana mtoto mmoja hivyo atakuwa mtu wa ajabu kama atakataa mtoto wake.

Azae bwana mi sikatai mtoto , maana mtoto ni baraka na ukizintaia mimi sina watoto wengi mimi hapa nina mtoto mmoja tu na nina tamani sana kuongeza familia ili wawe wengi kwaio yeye kama ana kibendi changu azae tu aache maneno mengi.

Maneno hayo ameogea petit man alipokuwa akiulizwa na soudt brown kwenye U-heard ambapo hayo yote yalikuja baada ya mange kimambi kuwa anamtukana mke wa petiti na kutoa siri kuwa wawili hao ndoa yao imekufa baada ya mwanaume wake kupata mke mwingine wa kinyrwanda  anaeishi Dubai.

Johari Adaiwa Kuwahi Kubanjuka na Petit Man

Msanii mkongwe katika tasnia ya Bongo Movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amedaiwa kuwahi kuonja Penzi la Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache.

Global Publishers wanaripoti kuwa waliwahi kubanjuka kipindi cha nyuma na hata juzikati walinaswa wakiwa kwenye uzinduzi wa filamu ya msanii Daud Michael ‘Duma’, Nipe Changu uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

Baada ya  picha ya wawili hao wakiwa pamoja Mlimani City kusambaa gazeti la Amani liliwatafuta na kufanikiwa kuzungumza na Johari huku Petit simu yake ikiita bila kupokelewa.

Jamani yule ni mshkaji tu na tukiwa karibu watu wanadhani tunatoka, sijawahi kutoka naye na sidhani kama ninaweza kufanya hivyo sababu ni mume wa mtu, naheshimu”.

Petit amemuoa dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz na pia Johari naye amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano na mwanamume mkoani Mwanza.

Petit Man Amjibu Billnass Kuhusu Kuondoka Katika Lebo Yao

Siku ya jana , msanii wa bongo fleva nchi Billnass alithibitisha kuwa kwa sasa hafanyi tena kazi na petit man na akasema kuwa aliyekuwa meneja wake huyo ameshaondoka katika lebo hiyo, akionekana asiye na wasiwasi billnass alipokuwa akiongea katika kipindi cha XXL, alisema kuwa Petit Man alisababisha damage kubwa sasa kwake kitu kilichofanya yeye kuona kuwa kuna  unafuu wa meneja huyo kuondoka katika lebo hiyo.

Hata hivyo watangazaji wa Clouds Radio hawakutaka kusikiliza upande mmoja hivyo waliamua kumtafuta kwa simu mhusika Peti Man ili aweze kujibu yake aliyoyasema Billnass kuhusu kusababisha athari kubwa kwa msanii huyo.

Peti Man alisema mimi ni moja ywa watu waliongia ghrama nyingi sana juu ya muziki wa billnass na ninaweza kusema kuwa yeye ndio kanitia hasara,lakini kwa sababu tulikuwa tukifanya kazi pamoja hivyo nilimchukulia kama mwanafamilia .siwezi kusem chochote kuhusu hilo lakini muda ukifika kila kiyu kitakuwa wazi.-Aliongea Petit Man kwenye simu.

Hata hivyo baada ya petit kuka ta simu, bilnass alisema kuwa hata kama damage hiyo inaweza isiwe ya pesa lakini bado alichokifanya kilim-cost sana.

Alipoulizwa Billnass kupitia kipindi hicho hicho, kuhusu mahusiano yake ya sasa na aliyekuwa meneja wake huyo bilnass alijibu kuwa hawana ugomvi wowte na wamekuwa wakisalimiana ingawa hawana ukaribu wa kikazi.

Tunda Amwita Petit Man Chawa Wa Wasafi

Mwanadada asiechuja ambae amekuwa akifanya vizuri mpaka sasa kutokana na kuuza sura katika video za wasanii mbalimbali ikiwemo video ya Diamond Platinumz  ‘Salome’, amemwita Petit Man mume halali wa Esma Platinumz kuwa ni chawa kutokana na kufatana fatana na Diamond na kundi la wasafi kila sehemu, ,Petit Man ni moja kati ya wanafamilia ya wasafi kwa sababu ni mume wa dada yake na Diamond anaejulikana kama Esma Platinumz.

Katika moja ya post katika kurasa za Dizzimonline, katika ukurasa wa instagram ambapo ilipostiwa picha ikimuonyesha Petit Man akiwa na mke wake Esma na Aunty Ezekiel akiwepo, Tunda alicoment na kumuita Petit Man kuwa ni chawa wa wasafi.

“Petiiman hatimaye amekuwa chawa wa WCB, kweli maisha yanabadilika” aliacha comment iyo katika picha, hata hivyo Petit Man na Tunda walikuwa wakionekana pamoja na hata kufanya kazi  pamoja lakini kinachshangaza mashabiki kuwa ni kwanini Tunda aandike ujumbe kama huo tena wazi katika post ambao watu wengi wangeiona au alijua kabisa kuwa lazima ujumbe utafika.

Hata hivyo , picha iyo ni moja ya picha zinazoonyesha matukio  na watu waliokuwa wameudhuria katika show mojawapo alioifanya Damond Platinumz  na Rayvanny katika uwanja wa Amani huko Zanzibar , Petit Man akiwa kama shemeji na mtu wa karibu wa familia ya Diamond alikuwepo kwa ajili ya kusapoti show hiyo.

Hata hivyo show iyo ilihudhuriwa na watu na wasanii wengi maarufu ikiwemo Aunty Ezekiel kutoka bongo movie, Zari The Bossy ambae baada ya kumaliza uzundizi wa  duka jipya Mlimani City mali ya Gsm waliondoka na kuelekea Zanzibar.

Hii sio mara ya kwanza kwa Petit Man na mkewe kutokea katika events na party za familai ya Diamond, na akiwa kama mwanafamilia na mtu anaesapoti sana muziki wa Tanzania basi anapotokea katika shughuli kama izo anakuwa pia na umuhimu wake kwa mkewe na kwa wasanii pia kwa sababu petit man alishawahi kuwa meneja wa wasanii mbalimbali wa bongo fleva na bado anaendelea kusapoti baadhi ya wasanii.

Tunda akiwa pamoja na Petit Man