Johari Akiri Mahaba Yake kwa Pombe

Mwanadada Johari chagula amefunguka na kusema kuwa katika maisah yake kitu kikubwa ambacho kimekuwa cha starehe kwake ni kunywa ppombe na wala sio kitu kingine.

Mwanadada huyo ambae aliwahi kuripotiwa hata kuibiwa akiwa baa amelewa anakiri kuwa starehe yake kubwa kwa sasa ni pombe na sio kitu kingine.

Akiongea na waandishi wa habari, johari anasema kuwa  aliamua kuchaguwa pombe kuwa starehe na rafiki yake mkubwa kwa sasa akiwa amekunywa pombe hakuna shida na mtu anayosababisha.

Hakuna kitu ninakipenda kama pombe, maana ndio starehe yangu pekee.

 

 

Johari Atokwa Povu Kuachana Kwa Ray na Chuchu hans

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amejikuta akimwaga Povu Baada ya kuulizwa kuhusu kuvunjika kwa Penzi la Vicent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hansy.

Wiki iliyopita habari zilisambaa kuwa Msanii Ray na Mpenzi Wake wa siku nyingi ambaye pia ni mama wa Mtoto wake Jaden, Chuchu Hansy wameachana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  na Risasi Jumamosi, Johari alisema kwa mwaka huu hataki kabisa kuzungumzia maisha ya Ray na Chuchu kwa sababu yuko bize na mambo yake ya maisha na si kuangalia familia za watu wengine hivyo wanaosema amefurahia wawili hao kumwagana wamuache.

Yaani sitaki kabisa kuzungumzia masuala ya hao watu, kwa sasa nipo bize na mambo yangu na pia hayanihusu na wala siwezi kusema kwamba sijafurahishwa kwa kuwa sihitaji kabisa kujua na kufuatilia maisha yao”. Johari ameshawahi kuwa kwenye mahusiano ya miaka mingi na Ray ingawa walikataa kuwahi kuwa kwenye mahusiano hayo kwa muda mrefu.

Johari Kufanya Maombi Baada Ya Kuandamwa na Mikosi

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Johari Chagula ameibuka na kudai kuwa ana Mpango wa kufanya maombi maalumu kwa ajili kuondoa mkosi ambao amedai umekuwa ukimuandama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Johari ameibuka na kudai ameamua kufanya maombi maalumu kutokana na mikosi ambapo amesema mwezi uliopita aliibiwa, alipata ajali ya gari hivyo kwake anaona si kawaida kwa hiyo anamuomba Mungu amuepushe na mabalaa ili aweze kumaliza mwaka vizuri.

Ulikuwa mwezi mgumu kwangu, nimepitia kwenye changamoto za mfululizo lakini namshukuru Mungu nipo imara. Nafanya maombi maalum Mungu aniepushe na mabalaa”.

Lakini pia mbali na kupatwa na majanga hayo mwezi uliopita kuna picha ziisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha akiwa amelewa chakari na taarifa kusambaa kwamba kwa hivi sasa ana tatizo la kunywa pombe kupindukia.

Johari Awekewa Madawa ya Kulevya Baa.

Mwanadada kutoka bongo movies Johari Chagula amekutwa na janga zito baada ya kuripotiwa kuwa aliwekewa madawa ya kulevya akiwa baa ambapo alionekana akiwa hapo akama akiwa anamsubiria mtu aliepanga kuonana nae.

Akitoa habari hiyo , mtu wa karibu wa Johari Chagula amefunguka na kusema kuwa nbaada ya kuwekewa madawa ya kulevya na watu wasiojulikana , watu hao walimuibia kila kitu na kumuacha mikono mitupu.

Akiwa anendelea kupata kinywaji kuna watu walikuja wakakaa pembeni yake ambao hata mimi sikuwajua lakini baada ya muda johari alikwenda chooni, lakini baada ya kurudi wale wtu walikuwa hawaonekanani tena pale maeneo ya karibu huku johari akiponekana kama kusinzia hivi.

Baada ya yeye mwenyewe kuzinduka alijikuta hana kila kitu na ndipo pombe ilipomuisha na kujikuta hana kitu hata kimoja na sisis tulihisi tu kuwa amewekewa madawa ya kulevya.

Baada ya hapo GPL waliamua kumtafuta Johari ambapo  alikiri kuwa alibiwa pochi iliyokuwa na simu pamoja pesa na vitu vyake vingine vya muhimu pamoja na kwamba hakuwajua watu waliomuibia.

 

Johari Adaiwa Kuwahi Kubanjuka na Petit Man

Msanii mkongwe katika tasnia ya Bongo Movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amedaiwa kuwahi kuonja Penzi la Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache.

Global Publishers wanaripoti kuwa waliwahi kubanjuka kipindi cha nyuma na hata juzikati walinaswa wakiwa kwenye uzinduzi wa filamu ya msanii Daud Michael ‘Duma’, Nipe Changu uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

Baada ya  picha ya wawili hao wakiwa pamoja Mlimani City kusambaa gazeti la Amani liliwatafuta na kufanikiwa kuzungumza na Johari huku Petit simu yake ikiita bila kupokelewa.

Jamani yule ni mshkaji tu na tukiwa karibu watu wanadhani tunatoka, sijawahi kutoka naye na sidhani kama ninaweza kufanya hivyo sababu ni mume wa mtu, naheshimu”.

Petit amemuoa dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz na pia Johari naye amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano na mwanamume mkoani Mwanza.

Siwezi Kumpenda Mwanaume kwa Sababu ya Pesa au Muonekano.:Johari

Mwandada Johari  Chagula amefunguka na kusema kuwa kamwe katika maisha yake haangalii muonekeno wa mwanaume ili kuwa nae katika mahusiano kwa sababu anajua kuwa  vitu kama hivyo vinatafutwa na muonekano kwake sio muhimu sana.

Johari ambae mpaka sasa hivi bado hajatangaza kuwa katika mahusiano wala kutaka kuolewa tangu alipoachana na Ray Kigosi na kuwa na mahusiano na Chuchu hans  anasema kuwa haja haja ya kuwa na mwanuem mwenye pesa wala muonekanao lakini anatamani kupata mwanaume mweny hofu ya Mungu.

Siwezi kumtaka mwanaume kutokana na muonekano wake au rangi yake,pia siwezi kumpenda kutokana na pesa maana hivyo vinatafutwa pia.mimi ninataka mwanaume anaejituma katika kutafuta lakini pia mweny hofu ya Mungu.

Duma Akiri Kumkubali Sana Johari

Msanii wa filamu za kibongo Daudi Michael maarufu kama Duma amefunguka na kukiri kuwa hakuna msanii wa kike anayemkubali kama anavyomkubali Johari.

Duma amekiri kuwa Msanii huyo mkongwe (Johari) ndio aliyempa yeye hamasa ya kuweza kuingia kwenye filamu miaka ya nyuma.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Duma amesema kuwa hata akiulizwa mahali popote kuhusu msanii aliyemfanya aingie kwenye uigizaji hawezi kuona aibu kusema ni Johari kwa sababu mpaka leo hii ndio msanii wa kike anayempenda sana.

Siwezi kuwa mnafiki hata kidogo ukweli ni kwamba Johari ndiye aliyenifanya niingie kwenye tasnia ya filamu kwa sababu alikuwa akiigiza kiuhalisia kwenye filamu yake ya Johari na mpaka leo ni mwanamke wa kwanza kumpenda Bongo Muvi“.

Johari alijizolea umaarufu miaka ya nyuma Kupitia maigizo kadhaa aliyokuwa anafanya na ambapo alikuwa anaigiza na wasanii kama Ray, Marehemu Kanumba na wengineo.

Johari Amtaka Hamisa Aachane na Diamond

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amempa somo mrembo Hamisa Mobetto kwa kumtaka aachane na Baba watoto wake Diamond Platnumz.

Johari amefunguka na kudai kuwa ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na staa hivyo anajua ni jinsi gani walivyo pasua kichwa hivyo anamshauri Mobetto aachane na Diamond.

Kwenye mahojiano  na Global Publishers, Johari amemtaka  Mobeto, asirudi kwa Diamond, bali angeendelea na maisha mengine maana kurudi ni kuambulia maumivu tu, hakuna cha maana zaidi.

Ningekuwa nimepata nafasi ya kumshauri Mobeto, ningemwambia asimrudie Diamond, lakini ndiyo hivyo nilisikia wako pamoja tena, ninachoweza kumwambia ni awe makini tu maana penzi na staa linaumiza sana. Kwani ni watu ambao hawatulii, atajikuta anajipotezea muda na baadaye kuja kujuta.

Nimewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa, uliniumiza sana na ndiyo maana nampa somo Mobeto kuwa makini sana ili kukwepa kuumiza moyo wake na kupoteza muda”.

Johari alishawahi kuwa na uhusiano wa muda mrefu na staa wa Bongo movie Ray Kigosi lakini walikuja kuachana na Ray kuzaa na Chuchu Hansy.

Inasemekana Kuwa Johari Ni Mjamzito

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kwa Jina la usanii kama Johari anadaiwa kuwa ni mjamzito kwa miezi minne sasa.

Global Publishers wanaripoti kuwa mtu wa karibu wa Msanii huyo amewapa taarifa hizo kwa sasa Johari ameongezeka umbo kwa sababu ya ujauzito alionao ambapo anafurahia kwani ni jambo alilokuwa akilitafuta kwa muda mrefu.

Mmemuona Johari kwa sasa? Ni mjamzito na mwenyewe ana furaha ingawa anaficha sana ili wapambe wasimharibie”.

Baada ya kupata habari nyepesi nyepesi hizo gazeti hilo lili mmvutia way a ili kujua kama taarifa hizo zina ukweli wowote ndipo Johari alipomwaga povu kidogo:

 Sipendi kuzungumzia hayo mambo yangu binafsi, kama mimba ipo mtaiona tu, lakini pia mimi ni mwanamke na umri wangu unaruhusu kuwa na ujauzito hivyo sioni tatizo“.

Johari tayari ni mama wa mtoto mmoja ambaye alimkubali kwa mara ya kwanza Miezi michache iliyopita baada ya kukataa kwa miaka mingi kuwa hana mtoto.

 

Johari Aipa Baraka Zote Ndoa Ya Ray na Chuchu Hansy

Muigizaji wa Bongo movie Johari Chagula ametoa baraka zake zote kwenye ndoa ya Ex wake Ray Vincent Kigosi na mama mtoto wake Chuchu Hansy.

Johari na Ray walikuwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi kipindi cha nyuma lakini ameibuka na kuweka wazi kwa hivi sasa hana kinyongo na wapendanao hao kuwa pamoja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Johari amedai kuwa hakuna kitu kitakachomfurahisha kama mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ akimuoa mzazi mwenziye, Chuchu Hansy.

Ray na  chuchu Hansy

Lakini pia Johari ameweka wazi  kuwa Chuchu ni chaguo sahihi la Ray maana ni mwanamke ambaye amemzalia mtoto mzuri.

Kiukweli nitafurahi sana mkurugenzi mwenzangu (RJ Company) akimuoa Chuchu. Kwanza ni mwanamke wa chaguo lake na pia amemzalia kidume cha nguvu na kwenye harusi nitakuwa mstari wa mbele“.

Ray na  Chuchu Hansy wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaden.

Johari Kuingia Rasmi Kwenye Siasa 2020

Msanii wa bongo movies Johari Chagula amefunguka na kuonyesha nia yake ya dhati ya kutaka kuingia katika siasa hasa mwaka 2020  huku akisma kuwa lazima atagombea  nafasi ya ubunge.johari atokuwa msanii wa kwanza kujiingiza katika siasa lakini inakuwa inategemea ni kwa kiasi gani anakuwa anataka kusaidia jamii yake.Akiongea katika kipindi cha kikaangoni Live cha Eatv, Johari alisema kuwa kamwe hawezi kuiacha ccma na  kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa ccm ni lazima aagombea ubunge  mwaka 2020.

nina mapenzi makubwa sana na chama changu cha CCM, na nina mpango mwaka 2020 nitagombe a ubunge na nia ninayo n apia uwezo ninao.sihitaji kiviongelea hivi vitu sana kwa sasa ila muda wa kuvifanya ukifika tu nitakuja kuviongelea.

Johari anasema kuwa hataki kuchanganya sana kazi zake za sanaa na mambo ya siasa kwa sababu mashabiki wake ni wa vyama tofauti na hataki kuwagwa hata kidogo.hivyo anaomba kuwa anapokuwa katika siasa atambulike kama blandina na akiwa katika sanaa basi ajulikane kama  Johari , jina ambalo limempa umaarufu katika sanaa.

Wasani wengi we waliowahi kuingia katika siasa ni pamoja na Irene Uwoya, Wema Sepetu ambao waligombea katika majimbo yao lakini kura za maoni hazikutosha hivyo walibaki kuwa wanachama wa kawaida .lakini pia kuna mwanadada Jokate ambae kupitia siasa ameweza kusaidia jamii yake kwa kutumia nfasi kubwa aliyonayo.

 

Johari Aongelea Safari Ya Kwenda Kumuona Lulu Jela

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Johari Chagula amefunguka na kuongelea sababu zilizompelekea kutomtembelea Lulu gerezani mpaka leo ilhali alifungwa tangu mwaka jana.

Elizabeth Lulu Michael ‘Lulu’ alihukumiwa kwenda jela mwaka jana tarehe 13/11 kwa muda wa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Muigizaji wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba.

Tangu Lulu ametupwa jela kumekuwa na taarifa nyingi juu ya nini kinaendelea kwa Lulu huko Lupango. Wasanii wengi waliokuwa na ukaribu na Lulu wamedai ni vigumu kwenda Kumuona jela kwani kuna sheria za kwenda hivyo wengi wao hawajamuona.

Johari amefunguka Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, na kusema tangu Lulu amefungwa hajawa za kwenda Kumuona wala kumuuliza hali kwani anaogopa kumuongezea machungu.

Kiukweli tangu Lulu amefungwa jela sijawahi kwenda kumsalimia, kwa upande wangu naona unapokwenda kumtembelea ni sawa na kumuongezea machungu na ukweli zaidi hivyo mimi ndio naona na ndio maana nakuwa mzito kwenda”.

Lakini pia Johari amesema kiitendo kilichowapata wote wawili kumaanisha Kanumba kufariki na Lulu kufungwa kiliwaumiza watu wote lakini ana wacha Mungu.

Johari Aamua Kuokoka na kutubu

Msanii mkongwe wa bongo movies Johari Chagula amesema kuwa ameamua kuokoka tena  na kuamua kuachana na mambo mabaya amabyo yatamigiza katika dhambi tangu kuanza kwa mwaka huu.Johari amesema kuwa ameamua kuwa karibu na Mungu kwa sasa kwaiyo anaachana na mambo yote yanayoweza kumfanya kuwa katika vishawishi ikiwa ni pamoja na kunywa pombe.

Johari amemwambia mwandishi kuwa amebini kuwa maisha ni mafupi sana kwiao ni bora kuanza kujisafisha mapema maana  na kujiweka karibu na Mungu kwa sababu mungu ndie mueza wa kila kitu.

ninaachana kabisa na mambo ya kiduia kwa sasa nilishafanya mambo mengi yasiyokuwa mazuri na hayakumpendeza Mungu , kama binadamu ninaanza kujipanga  upya na ninasema kabisa kuwa nimeokoka. Alisema Johari Chagula.

Swala la kuokoka kwa Johari au mtu mwingine yoyote inategemea na imani ya mtu huyo hivyo kwa watuwaliopo nyuma yake , tunamtakia kila lenye kheri kwenye maisha mapya ya uokovu.

Johari Akiri Kupata Raha Enzi Za Uhai Wa Ndikumana

Akiwa kama rafiki wa karibu wa msanii mwenzie , Johari Chagula amefunguka na kukiri kuwa enzi za uhai wa marehemu Ndikumana walikuwa wakila bata sana.Johari ambae ni rafiki wa karibu wa Irene Uwoya alisema kuwa kipindi Irene Uwoya  alipokuwa bado hajagombana na mumewe marehemu Ndikumana walikuwa wakila bata sana hasa pale Ndikumana alipokuwa akitoka nchini kwao akija Tanzania.

Johari anasema kuwa hata alipokuwa akija nchini alikuwa akija na zawadi nyingi kwa ajili ya marafiki wa karibu wa mkewe , na kuna kipindi mpaka waliweza kusafiri mpaka Cyprus kwa ajili ya kula bata tu na kurudi Tanzania.

kwakweli kama unavyojua mimi na Irene damudamu,Ndikumana alikuwa akitupa raha hatari hatari.Kuna wakati tulienda  naye hadi  Cyprus tukala raha sana.Kweli ndiku alikuwa na roho ya peke yake sana,Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Alifunguka Johari Chagula

Ndikumana alifariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa moyo uliomkuta ghafla alipokuwa akiendelea na shughuli zake.hata hivyo sio wasanii wote wa bongo waliofanikiwa kuhudhuria katika mazishi yake kwa sababu hayakufanyikia nchini tanzania lakini familia ya Irene Uwoya pamoja na kwamba wawili hao hawakuwa katika maelewano mazuri kutokana na Irene kuolewa ndoa ya pili ya kiislamu kabla hata ya kuachana na Ndikumana  walifanikiwa kuona kaburi la msanii huyo.

Siku chache zilizopita, moja ya wadogo wa Ndikumana anaejulikanakama Laddy Ndikumana aliwatukana wasanii wa bongo movies na kuwahita wanafiki kwa kile kilichodaiwa kuwa kipindi marehemu yupo hai walikuwa wakila nae bata lakini marehemu amefariki hakuna aliyejitokeza katika msiba.