Rommy Jones Aanika Kilichomvuta Kwa Kay

Kaka na official Dj wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Romeo Jones maarufu kama Rommy Jones amefunguka na kuanika sababu zilizopelekea mpaka kufunga ndoa na mpenzi wake Kijoli au maarufu kama Kay.

Rommy Jones alifunga ndoa na Kay mwaka jana mwishoni baada ya kuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global PublishersRommy alisema kuwa mkewe huyo alionesha uvumilivu mkubwa enzi za uhusiano wao na ndipo alipobaini kuwa, ndiye mwanamke sahihi wa kumpa heshima ya ndoa.

Niliamua kuoa kwa sababu niliona uvumilivu wa mwanamke huyo kwani nilimfanyia madudu mengi lakini alinivumilia. Kuna wakati nilikua aondoka nyumba na kurudi baada ya siku tatu nikiwa nimelewa lakini alinivumilia, nikabaini huyu ndiye mwenye sifa ya kuwa mke wangu”.

Barakah The Prince Akubali Msamaha Wa Rommy Jones

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amekubali msamaha alioombwa na Rommy Jones baada ya kumtongoza mpenzi wake Naj na kisha kumponda Barakah.

Stori hii ilitengeneza headlines wiki iliyopita baada ya meseji za Rommy Jones alizokuwa anamuandikia  Naj kumtongoza kuvujishwa Kwenye mitandao ya kijamii jambo lililozua kizazaa hasa kwa sababu Rommy alikuwa ametoka kuoa na Naj ana mpenzi.

Lakini Kwenye meseji hizo Naj alimkataa Romy na kumwambia anampenda mpenzi wake Barakah lakini cha ajabu alianza kumponda Baraka na kumquat king’asti na pia kusema anazima nyota yake amuache ili akawe mchepuko wake.

Barakah alimjia juu Romy na kuhaidi kumuuliza endapo wakikutana Lakini jana Romy kamuomba msamaha Barakah na bila hiyana Barakah kakubali msamaha Ule na kamtaka wafanye kazi.

Kupitia mtandao wa Instagram Barakah aliandika maneno haya baada ya kuombwa msamaha:

Ni vyema sana Mtu kutambua kosa lake na kutubu..Na anapoomba Msamaha anapaswa kusamehewa..Sina noma na wewe bro,Tupige kazi man”.

 

Rommy Jones Amuomba Mkewe Msamaha Baada Ya Kuchepuka

Msanii na Dj maarufu Rommy Jones ambaye pia ni kaka wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemuangukia kwa magoti mke wake Kay Jord na kumuomba msamaha mtandaoni baada ya kukamatwa akitaka kuchepuka.

Wiki iliyopita Rommy jones alitengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii baada ya meseji zake za kumtongoza Naj kusambazwa mtandaoni Ikiwa ni Miezi michache tu tangu ametoka kumuoa mke wake.

Jana Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rommy Jones ameandika ujumbe wa kumtaka radhi mke wake kwa kitendo hiko pamoja na kwamba alikataa kuwa alimtongoza Naj na kudai ilikuwa ni utani tu:

Baada ya kuombwa msamaha mke wa Rommy ambaye na yeye alikuwa ameshafuta picha zito za Rommy Kwenye ukurasa wake wa Instagram aliweka picha yao ya Harusi na kuisindikiza na ujumbe uliosema “Pale Shetani alipotujaribu na akashindwa”. Kuashiria wamesha samehana na kuendelea mbele.

 

Mke wa Rommy Afunguka Mazito Baada Ya Mumewe Kumtongoza Naj

Wiki iliyopita Rommy Jones alizua gumzo baada ya meseji zake alizomtumia msanii Naj kwa ajili ya kumtongoza kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

Jambo hilo lilizua mambo mengi kwa sababu Rommy ametoka kuoa miezi michache iliyopita kwaiyo kitendo cha yeye kumtaka mwanamke mwingine kilishangaza wengi.

Lakini tangu siku ya Ijumaa mke wa Rommy Jones anayejulikana kama Kay Jord aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuachana na mume wake kwa sababu ya michepuko.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda mke wa Rommy amefunguka na kudai meseji hizo zilizodaiwa kwamba mumewe alikuwa akimtongoza Najma, haziendani na ukweli kwani asilimia kubwa zilionekana ulikuwa ni utani:

Nimesikia na watu wamesema mengi kuwa mimi nimeondoka nyumbani, kisa hizo meseji, jambo ambalo siyo kweli kabisa.
Hakuna ukweli kwenye jambo hilo ndiyo maana niliamua kukaa kimya”.

Kwa upande wake, Rommy alilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, yeye ni mfanyabiashara na Najma wanafahamiana vizuri.
Alisema kuwa, kuhusiana na hizo meseji anazodai kumtongoza Naj ilikuwa ni utani wa kawaida tu.

Baada Ya Rommy Jones Kumtongoza Naj, Mkewe Kasema Hana Mpango Wa Kumuacha

Siku ya leo Romy Jones ambaye ni kaka wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameingia kwenye headlines baada ya meseji zake akimtongoza msanii wa Bongo fleva Naj kuvujishwa Instagram.

Kwenye meseji hizo Rommy anamtaka Naj ambaye ana  uhusiano wa kimapenzi na Msanii wa Bongo fleva Barakah The Prince ambapo amemponda na kudai Barakah anashusha nyota yake.

Rommy Jones alimuoa mkewe Miezi michache iliyopita ambaye anajilikana kama Kay Jord kwaiyo baada ya skendo yake ya kumtaka Naj ambaye pia ni Ex wa kaka yake Diamond kutokea iliwashangaza watu wengi.

Baada ya sakata hilo kutokea asubuhi hii Kay ametumia ukurasa wake wa Instagram kujulisha watu kuwa hana Mpango wa kuachana na mumewe ambapo ametumia msemo unaosema:

Kumuacha mwanaume kisa anaku cheat ni sawa sawa na kukimbia nchi kisa mvua inanyesha kwani mvua hunyesha kila sehemu”.

Akimaanisha wanaume wote wanachepuka hivyo hawezi kumuacha mumewe kisa na mjadala kachepuka.