Nilimkataza Mke Wangu Kujiboost Kabla ya Shoo :-Uchebe

Kuna baaadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakifanya ama desturi kubwa pombe kabla ya shoo kwa ajili ya kujiboost na kuondoa aibu ya kupanda juwaani ili kuwa-face mashabiki.

Kumbe hii pia ilikuwa ni tabia ya mwanadada Shiloleh ambae ameuwa akinywa pombe kabla ya shoo ili kuwaface mashabiki, sasa basi mume wa msanii huyo anafunguka na kusema alimkataza kabisa mwanadada huyo kufanya hivyo.

Wakiongea katika kipindi cha Leo tena cha Clouds Media, Uchebe anasema kuwa aliamua kumtaza kabisa mke wae kufanya hivyo na kumtaka kuwa kama yeye pale anapoenda kukutana na mashabiki zake ili kujua uwezo wae kwa mashabiki, lakini hiyo pia inamfanya utofanya vitu vya aibu ambayo mwisho wa shoo anaweza  kujta kwanini alifanya.

Nilimwambia usitumie kilaji chochote abla ya kupanda jukwaani, anasema asipokunywa anaona watu sio wengi, nashukuru Mungu wa sasa hafanyi hivyo tena na hata akinywa ni kiasi kidogo sana.

Uchebe Akana Kumpiga Shiloleh.

Mume wa msanii Zuwema Mohamed maarufu kama Shiloleh anaejulikana kama Uchebe amefunguka na kuongelea swala la yeye kumpiga mwanamke wake baada ya kusambaa kwa maneno katika mitandao ya kijamii kuwa inawezekana wawili hao wamegombana baada ya kutokea kwa ugomvi mkubwa ambao ulisababaishwa na Sudy Brown.

Uchebe anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakimuona kaka yeye mi mtu baunsa na kwamba anaonekanakuwa anampiga mke wake kila siku lakini ukweli ni kwamba hajawahi kumpiga mke wake huyo hata siku moja tangu amemuoa na maneno yanayosema hayana ukweli wowote.

Watu wengi wananiona kama mimi ni mtu wa kupiga piga tu,lakini ukweli ni kwamba siwezi kumtandika mke wangu hata siku moja.-Alifunguka Uchebe

Waandishi wa habari waliamua kumtafuta Shiloleh ili kumuuliza kama zile habari za kuwa wanaugomvi na mume wake na kwamba alipigwa hadharani kama zina ukweli wowote , lakini shiloleh alikataa na kusema kuwa hakuna kitu kama icho.

Shiloleh:Sitakubali Mume Wangu Aoe Mke wa Pili.

Msanii wa muziki nchi na mjasirimali maarufu bongo kwa upande wa  wanamuziki ambae amekuwa akijituma sana katika kufanya kazi na kujilindia heshima yake mjini , Shiloleh amefunguka na kusema kuwa kamwe katika maisha yake haitakuja kutokea kumruhusu mwanamume wake kuoa mke wa pili eti kwa sababu anataka kusaidiwa majukumu.

Shiloleh anasema kuwa hakuna kitu kigumu kama ndoa ila watu tu hawajui, na kama mwanaume anashindwa kuyatuliza maswala yake katika ndo ya mke mmoja hawezi kutuliza kwa ndoa ya pili.Shiloleh anasema kuwa kamwe mume wake hatooa mke wa pili na hata yeye hawezi kukubali hata kama dini yao inaruhusu kwa sababu hata hiyo dini kuna mambo inataka mwanaume atimize akioa mke wa pili.

mimi mume wangu hawezi kuoa mke wa pili hata kama dini inaruhusu , na anaoa mke wa pili for how,mimi nina mapungufu gani kwanza mpaka aoe mke wa pili.mtu mwingine anaweza kuwa na mapungufu yake na huwezi kuyajua.kwaio mimi sina mapungufu yoyote.me wangu kamwe hawezi kuoa mke wa pili  hata kama dini inaruhusu hata hiyo dini inavyoruhusu kuna mambo anatakikana kuyajua na kuyafanya.

Mwingine anakwambia eti kuoa mke wa pili mbona kawaida tu,je unaweza kuyafanya yanayotakiwa ndani ya ndoa au, sio unaiona ndoa tu jamani ndoa ngumu.hawezi kuoa mke wa pili hata kama dini inaruhusu na kamwe sitakaa nikubali aoe mke wa pili.

Maneno ya Shiloleh ayankuja baada ya mwandishi wa Ayo Tv kumuuliza maoni yake kuhusu kile kilichosambaa katika mitandao wiki iliyopita  baaada ya mkuu wa Wilaya ya Pangani kuweka wazi kuwa yeye ndie aliyemruhusu mume wake kuoa mke wa pili ili aweze kumsaidia majukumu amo mume wake anakosa pindi anapokuwa katika majukumu ya kikazi serikalini.

Shiloleh na Uchebe wanatimiza zaidi ya miezi mitatu sasa tangu kufungwa kwa ndoa yao mwaka uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi maarufu na kupewa zawdi mbalimbali katika harusi yao.

Baba Levo Atoa Tahadhari Kwa Nuh Mziwanda na Nedy Music juu ya Shilole

Ikiwa ni siku kadhaa tu zimepita tangu msanii wa muziki bongo Zuwena maarufu kama Shiloleh kufunga ndoa, aliyekuwa Mc katika harusi yao ambayo ilifungwa mwaka jana na haruis kufanyika mwaka huu January 14 amefunguka na kuwataka wasanii wenzake ambao walikuwa na mahusiano na Shiloleh kutulia na kuacha usumbufu kwa mwanamke huyo kwa sababu alishaolewa na hawezi kurudiana nao tena.

Baba Levo ameswataja wasanii hao kuwa ni Nedy Muisc  pamoja na Nuh Mziwanda ambao walikuwa wana mahusiano na Shiloleh hapo mwanzo kabla ya shiloleh kuwa na uchebe ambae ameamua kufunga nae ndoa.

Baba Levo amewaambia wasanii hao kuwa watumie kigezo cha kimapenzi yao ya nyuma kuwa karibu na Shiloleh kwa sababu sasa hivi shiloleh ni mke wa mtu na endapo watakuwa wanaonekana kunyapia nyapia kwa shiloleh watapigwa makofi na uchebe.

na kuanzia sasa hivi shiloleh naomba utulie na kumuheshimu mume wako ambae umeamua kuanza nae maisha , na kwa hiki kinachotokea sasa hivi naomba nedy music na nuh mziwanda muache kumfatilia shiloleh uchebe amekomaa atatupiga makofi, atawapiga makofi na biashara inaishia hapo.

Shiloleh alishawahi kuwa na mahusiano na wanaume hao kipindi cha nyuma kabla ya kuolewa na uchebe ambapo kwa upande wa nuh mziwanda amekuwa akimsumbua na kumkebei Uchebe hata baada ya kutangaza kufunga ndoa na Shiloleh.

Wasanii wengi wamekuwa wakitilia mkazao swala la wanaume wa nyuma wa mwanadada huyo kumuacha Shiloleh kufanya maisha yake mapya ya ndoa yawe ya amani huku wengi wao wakiwataaharisha kumuogopa Uchebe ambae anaonekana kuwa mkali.

Harusi Ya Shiloleh na Uchebe Ilivyofana.(Picha)

Sherehe ya msanii  Shiloleh na mume wake Uchebe imefanyika jana tarehe 14 katika moja ya kumbi zilizopo masakai jijini Dar Es Salaam.Sherehe hiyo imefanyika baaada ya wawili hao kufunga ndoa takribani mwezi umepita na kuifanya ndoa hiyo kimya kimya bila kuharika watu hivyo siku ya jana waliamua kufanyasherehe ili kuweka kujumuika na baadhi ya watu wao wa karibu  pamoja na mashabiki zake.

Muda mchache baadaya kuingia ukumbini .

Uchebe akimvisha pete mkewe Shiloleh.

Mtu na mkewe wakikumbatiana.

Shiloleh na Uchebe wakubusiana mbele ya mashabiki ukumbini katika hafla hiyo fupi.

Baadhi ya watu maarufu waliohudhuria party hiyo akiwepo Diamond Platinumz, Wolper , Harmonize na mkewe .

 

Ndoa Ya Shishi na Uchebe Yafungwa Kimya Kimya

Ile ndoa iliyokwa ikisuburiwa kwa muda mrefu ya msanii wa bongo fleva Shilole na mumuwe uchebe hatimaye imefanikiwa kufungwa baada ya kupata misukosuko  kwa muda kidogo. Ndoa iyo iliyofungwa jana usiku ilifungwa kimya kimya huku ikisemekana kuwa iliudhuriwa na watu kumi na tano tu huku ikisemwa kuwa hakuna hata msanii mmoja aliyehusishwa katika ndoa iyo isipokuwa Babutale  meneja ya msanii Diamond ambae ndiie aliyewakilisha upande wa wazazi wa mwanamke.

Hata hivyo ndoa io imewaacha watu wengi midomo wazi kutokana na muda ndoa iyo ilipofungwa na kufungwa kimya kimya bila kualikwa kwa watu ilhali Shiloleh aliahidi kuwa siku ya ndoa yake  angependa watu wajae na wasitoe mchango wowote.

Shilole na Uchebe walianza mapenzi yao kwa muda wa zaidi ya miezi tisa sasa huku Uchebe akitoka kwenye ndoa yake ya kwanza ambayo alimpa talaka mkewe na kuhamia kwa Shilole , hata hivyo wawili walishaanza kutangaza dhumuni la kufunga ndoa iyo kwa muda mrefu na sasa wamefanikisha swala hilo.

Ingawa hivi karibuni zilivuja picha za Shilole na mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda ambazo zilifanya watu waamini kuwa uwezekeno wa ndoa iyo kuwepo nimmodgo lakini hatimaye wawili ho wamefanikiwa kuziba watu midomo na kufanikisha adhma yao.KILA LENYEKHERI KWAO.