“Tanasha Ndiye Mwanamke Pekee Mwenye Sifa Za Kuoa”- Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini na Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz ameibukana na kumwagia sifa lukuki Mpenzi Wake Tanasha Donna Oketh mwenye asili ya Kenya.

Diamond ameonekana kuzidi kunogewa na Penzi la Tanasha kwani amedai kuwa yuko tofauti na wanawake wote aliowahi kuwa nao hapo nyuma na kudai yeye ni ‘Wife material zaidi’.

download latest music    

Zikiwa ni Wiki mbili tu zimepita tangu Diamond atangaze rasmi ndoa na Tanasha Diamond anaonekana hakuwa na masihara kuhusu jambo hilo kwani kwenye interview yake na kituo kimoja cha habari nchini Kenya Diamond alisema haya:

Tanasha ndiye mwanamke pekee aliyeonesha kujali na uzito juu ya jambo hilo hivyo rasmi natangaza kumuoa huyu. Ana sifa zote za mwanamke wa kuoa, lakini unajua sisi wanaume wengi huwa tunaangalia sura, umbo na vingine vya mwilini kisha ndiyo inafuata tabia. Lakini nimejiridhisha kwamba mbali na umbo na mvuto wa kipekee pia ni mwanamke mwenye tabia nzuri”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.