Tanzia: Mama Mzazi Wa Lady Jay Dee Afariki Dunia

Mama mzazi wa staa mkongwe wa Bongo fleva Judith Mbibo maarufu kama Lady Jay Dee anayejulikana kama Martha Mbibo, amefariki dunia alfajiri ya  Alhamisi Aprili 26, 2018.

Taarifa hizo zimetolewa na Kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, ambaye amethibitisha na amesema kwamba mama yao amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua Saratani kwa muda mrefu.

download latest music    

April 01, 2018 Lady Jaydee alizungumza kuhusu kuugua kwa mama yake mzazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika;

Nauguza mama mzazi lakini naendelea kupambana na maisha vilevile, usinione naimba au natabasamu ukafikiri nina raha sana.

Sina raha wala nini, lakini pia lazima nifanye kazi ili niweze kuishi, bila kuangalia kama watu watani judge vipi!, Kwani bado naamini Mungu atamponya na kumnyanyua kwenye kitanda alicholala kwa zaidi ya miezi 2, Kwani Mungu pekee ndio anaeweza.

Bi. Mbibo alianza kuugua tangu mwishoni mwa mwaka 2016 ambapo alipatiwa matibabu hapa nchini na nje ya nchini (India).

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.