Loading...

Tiko Aogopa Kutapeliwa , Aajiri Mwanasheria Wake.

May 16, 2018 at 09:36
Tiko Aogopa Kutapeliwa , Aajiri Mwanasheria Wake.

Mwanadada Tiko Hassan kutoka bongo movies amefunguka na kusema kuwa tangu Mh waziri Harrison Mwakyembe alipokuwa akiwapigia kelele wasanii kuhusu kuangalia sana wanapofanya mikataba na makampuni mbalimbali kuwa makini ili wasitapeliwe na yeye amepata akili sasa ya kutafuta mwana sheria wake ili kuogopa kutapeliwa.

Tiko anasema kuwa kwa sasa kila kazi anayotakiwa kuifanya ni lazima amshirikishe mwanasheria wake ili kuepuka kuzurumiana na kuwa kutapeliwa na watu kama unavyofanyika kwa wasanii wengine wanaofanya kazi isiyokuwa na faida.

Loading...

Unajua watu wamekuwa wakitumia nafasi ya njaa zetu kutudidmiza na kutusainisha mkataba ya ajabu hivyo tumeshtuka baada ya waziri wetu kulizungumzia hilo bungeni, nna kuchukua tahadhari mapema hivyo kwa sasa nina mwanasheria wangu kabisa  na meneja ambao wananisaidia katika kila kitu kwaio sio rahisi kuingizwa mkenge.-Alisema Tiko alipokuwa akiongea na Global Publishers

Tiko anasisitiza pia wasanii wengine kuwa makini na swala la kufanya mikataba kwa makubalino yasiyofuata sheria husika.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…