Tunda Adaiwa Kuzama Kwenye Penzi Zito na Tajiri Mtoto

Video vixen asiyeisha vituko kwenye mitandao ya kijamii Anna Kimario maarufu kama Tunda amedaiwa kuwa kwenye penzi zito na kijana mwenye mkwanja mrefu anayejulikana kama Tajiri mtoto.

Global Publishers wanaripoti kuwa, Baada ya kumwagana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kisha kuhamia kwa mtangazaji wa Clouds TV Casto Dickson, Tunda amemnasa jamaa anayefahamika kwa jina la Tajiri Mtoto wa Arusha anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 27.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Jumamosi ndugu yake Tunda ambaye ameomba hifadhi ya jina, alidai kuwa kwa sasa video queen huyo anatoka na kijana huyo anayefanya kazi kwenye migodi na kwa kuwa ana mkwanja wa kutosha, Tunda ameamua kuhamishia makazi yake Arusha.

Tunda kwa sasa anaishi mjini Arusha, amepata bwana mwenye fedha zake watu wanamuita Tajiri Mtoto kwani ana hela za mgodini zinamsumbua, wanaume wa Dar watamsikia tu na kumuona mitandaon”.

Baada ya tetesi hizi kusambaa gazeti hilo lilimsaka tunda na kumhoji kuhusiana na tetesi hizo ambapo alifunguka;

Nimehama ndio maisha ya Dar si yangu tena kwa sasa nina maisha mengine na kifupi sipendi sana kuanika mambo yangu naomba watu waelewe hivyo kama wanavyoniona mitandaoni”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.