Uhusiano Wa Ben Pol Na Ebitoke Wafikia Pabaya

Msanii wa kiume wa muziki wa Bongo Fleva nchini anaefanya vizuri katika muziki na katika jukwaa la fiesta, tamasha kubwa linaloendelea kwa sasa katika baadhi ya mikoa mbalimbali. Ben Pol , ambae pia mashabiki wengi wanamwita “king of RnB”, ambae pia  ilisemekana yeye  kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msanii chipukizi wa vichekesho nchini  anaejulikana kama Ebitoke wameingia katika vichwa vya habari tena baada ya mahusiano yao kuonekana kusuasua.

kwa kipindi kirefu cha nyuma wasanii hao walionekana kuwa pamoja baadhi ya maeneo na kukiri kuwepo kwa ukaribu kati yao.Ingwa mara nyingi msanii huyo wa kiume Ben Pol alikuwa akikiri kuwa ukaribu wake na msanii Ebitoke ni wa kikazi zaidi kwasababu Ebitoke bado ni msanii chipukizi hivyo anahitaji msaaada katika kazi zake ili aweze kujulikana katika kazi zake, ilhali wakati huo huo msanii huyo wa kike Ebitoke alikuwa akisema kuwa yeye na Ben Pol wana mahusiano ya kimapenzi na anampenda sana na Mungu akiwajalia basi watafunga ndoa na kutengeneza familia pamoja.

download latest music    

Ni kama week imeyopita tu ambapo msanii Ebitoke alikuwa akihojiwa katika kituo cha televisheni cha EATV, alikuwa akilalamika kuwa  kwa muda sasa kumekuwa na mawasiliano yasiyo mazuri kati yake na msanii Ben Pol, akiendelea kuongea, Ebitoke alisema kuwa akimtumia Ben Pol sms hajibu wala akimpigia Ben Pol hapokei simu zake.Hata hivyo ebitoke aliendela kusema  na kusisitiza kuwa yeye bado anampenda sana Ben Pol na alitaka kujua kwanini Ben hapokei simu zake wakati walikuwa na mipango mingi, ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika kazi zao.

Hata hivyo baada ya msanii Ben ol kutafutwa ili aweze kujibu tuhuma hizo Ben Pol alikuwa akionekana kukwepa swala ilo na kusema kuwa  issue za Ebitoke zinamkata stimu”sasa hivi niko busy sana, kwa sababu nafanya mazoezi ya show,lakini kiukweli habari za Ebitoke zinanikata stimu kabisa, so  nikitulia ninaweza kukucheki”alisema Ben Pol ambae kwa muda sasa amekuwa akikwepa maswali ya waandishi wa habari yanayomuhusu Ebitoke.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.