Vanessa Mdee Afunguka Baada Ya Kuimba Nyimbo Ya Kihindi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee ameibuka na kuanika ugumu alioupata baada ya kuandika na kuomba wimbo wake wa Kihindi unaoitwa ‘Vaishnav Jan’.

Katika mahojiano yake na Risasi Vibes, Vanessa amedai kuwa alifuatwa na ubalozi wa India ambao upo Tanzania ili autunge na kuuimba wimbo huo kwa ajili ya kutumika kwenye maadhimisho ya miaka 150 ya kufariki kwa baba yao wa Taifa, Mahatma Gandhi ambayo hufanyika kila mwezi Oktoba huko India.

download latest music    

Orijino wa wimbo huu umefanywa na msanii wa kwao wa zamani sana wa kike, sasa katika kuadhimisha miaka hiyo 150 wakaona watafute mtu mbadala wa kufanya kava kwa ajili ya kucheza pamoja na video ndipo wakanipata mimi,” alisema Vee Money na kuongeza“.

Kwa hiyo kutokana na fursa hiyo nikafanya wimbo nikiongoza na mwalimu wa lugha ya Kihindi na tukashuti video ndogo ambayo ipo Youtube. Ilikuwa kazi kwani Kihindi sijui lolote hata ukinitukana lakini kwenye kuimba nimefanya vizuri na tayari nimepokea barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje India, Swaraj akinipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanya“.

Baada ya kuimba wimbo huo serikali ya India ilimtumia barua  ya shukrani na kuonyesha kufurahishwa na wimbo ule.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.