Vanessa Mdee Amaliza Bifu Lake na Mimi Mars

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money amefunguka na kuweka wazi kuwa ameamua kumaliza bifu lililokuwepo kati yake na mdogo wake ambaye pia ni msanii mwenzake Mimi Mars.

Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa yeye pamoja na ndugu yake huyo kama ilivyokuwa katika familia yoyote kulikuwa na migongano lakini amefikia uamuzi wa kumaliza bifu hilo na kwa sasa wako vizuri.

download latest music    

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Vanessa Mdee Vanessa amesema kuwa ameamua kumaliza tofauti kati yake na ndugu yake huyo kwa kuwa wao ni ndugu hivyo hakuna maana yoyote wao kutofautiana.

Naona ni jambo jema kwa kuwa mimi na mdogo wangu tulikuwa hatupo pamoja kutokana na sababu tu ambazo hazina msingi. Kwa hiyo nimeona tumalize bifu letu na tuendelee kupeana sapoti katika kazi zetu japokuwa kila mmoja anafanya muziki wake“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.