Vanessa Mdee na Ndoto Yake Ya Kusambaza Viatu Vyake Afrika

Staa wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ameibuka na kuweka wazi kuwa Hivi sasa Ndoto Yake kubwa ni kuviona viatu vyake vinasambaa Afrika nzima.

Vanessa ambaye hivi karibuni alizindua bidhaaya viatu vyake vya kike hususani kwa wanafunzi, amesema yupo kwenye mchakato wakuvisambaza Afrika nzima.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Vanessa Mdee amesema kuwa moja ya mikakati ya kupanua soko la bidhaa za viatu vyake ni kuviuza  nje ya Tanzania.

Nategemea brand yangu kuipanua zaidi na ili ikue nategemea kupata masoko katoka nchi mbalimbali za Afrika, lengo ni kuwafikia wanafunzi wengi wa shule za kiafrika“.

Viatu hivyo vinapatikana katika maduka  mbali mbali nchini Tanzania na vinafanya vizuri kwenye mauzo  yake sokoni.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.