Vera Sidika Athibitisha Kufanya Ngoma WCB

Mrembo anayetrend hivi sasa kutoka nchini Kenya Vera Sidika ‘Queen Vee’ ambaye hivi karibuni ameingia kwenye tasnia ya kuimba ametangaza kufanya ngoma yake ya pili ndani ya WCB.

Wiki iliyopita Vera alitengeneza headlines Baada ya kuachia wimbo wake ‘Nalia’ ambao ndani yake Alionekana model Calisah Kama video vixen.

download latest music    

Mpaka sasa Wimbo wa Vera unafanya vizuri sana kwani umepata watazamaji zaidi ya Laki Sita ndani ya Wiki moja na unatrend namba moja kwenye mtandao wa YouTube nchini Kenya.

Lakini hivi sasa Vera amekwisha tangaza ujio wa single yake mpya ambayo ameifanya na mtayarishaji wa muziki wa Label ya Wasafi WCB Laizer.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vera ametangaza habari hiyo njema na kuandika:

Nani yupo tayari kwa ajili ya wimbo wangu mpya nilifanya Wiki iliyopita ambao umetayarishwa na producer mkali kutoka Wasafi Laizer?….Nitauachia pale tu Naliawutakapofikisha watazamaji milioni moja”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.