Wanaume Watano Wamejitokeza Wanataka Kunioa- Wema

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kueleza jinsi wanaume wanavyomiminika kwao kutaka kutoa posa ili wamuoe.

Wema amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda ambapo amedai kuwa kuna muda wanaume watano tofauti walienda kutoa posa kwao lakini aliwakataa wote:

download latest music    

Walijitokeza karibu wanaume watano wanaenda, kwa mama kupeleka barua kinachotokea mama ananiita, ananiuliza mimi, sikubali kwa sababu siwezi kuolewa na mtu ambaye simjui au sijakaa naye“.

Lakini kuhusu Kuolewa hivi sasa Wema amejibu hawezi kuweka wazi lakini ana mpenzi wake ambaye anampenda lakini hawezi kumuweka wazi kwani amekuwa mtu mzima siku hizi.

Wema amefunguka na kumpongeza msanii wa Bongo fleva ambaye pia ni rafiki yake wa karibu Ali Kiba kwa kufunga ndoa hivi karibuni ambapo amesema:

Ninampongeza sana kwa mwanamuziki mkubwa kama yeye kufanya jambo hilo amejijengea heshima kubwa sana, lakini ninaamini mke yupo popote ni jinsi tu Mungu alivyokupangia wapi utampata“.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.