Wema Ni Mkorofi Kutoka Ndani -Martin Kadinda

Mwanamitindo maarufu nchi Martin Kadinda ambae pia ni mtu wa karibu wa Wema Sepetu, amefunguka na kusema tabia za Wema ambazo inawezekana mashabiki wake  wamekuwa hawajui kuhusu yeye.Martin Kadinda anaasema kuwa kwa watu wasiomjua wanaweza kusema Wema ni mpole lakini ukweli ni kuwa Wema ni mkorofi sana kuliko vile watu wengi wanavyoweza kuamini.

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, mwanamitindo huyo amesema kuwa  Wema Sepetu yupo tofauti sana na vile watu wanavyomfikiria na kumuona kwenye mitandao ya kijamii, kwa sababu yeye anamjua Wema vizuri kuliko mtu yoyote na hivyo huwa anajua kabisa pale anapogombana na mtu kuwa Wema ameguswa wapi mpaka amefikia hatua ya kuongea maneno hayo.

download latest music    

wema ni mkorofi kutoka ndani kabisa,lakini huwa anajitahidi kadri ya uwezo wake na nguvu zake zote ili ukorofi ule usionekane,lakini pia akiamua kukorofisha anakorofisha kwelikweli,kuna matukio mimi nakisikia anafanya tu najua kabisa hapa wema ameguswa wapi” Alisema Martin

Hata hivyo Martin anaendelea kusema kuwa Wema Sepetu ni mwanadada ambae ana moyo wa huruma sana na anapenda sana kuongeza marafiki kiasi kwamba huweza kumuamini mtu yeyote hata kama bado hajamjua vizuri  “lakini pia kitu kingine ambacho Wema anacho ni open door,milango ya moyo wake iko wazi sana, na yuko wazi kiasi kwamba anaweza kumuamini mtu yeyote,mtu yeyote anaweza kuaj kwake na akwa rafiki yake na akalala hata kwake” aliongea Martin Kadinda

Martin ambae amekuwani mtu  karibu zaidi na Wema kuliko mtu yeyote yule, amekuwa ni moja ya watu wanaojitahidi kumuongelea sana Wema hasa pale watu wanaongea maneno tofauti na vile alivyo,kuna kipindi Martin alishawahi kusikika akisema kuwa  ni vigumu kufanya kazi na Wema kwa sababu Wema ni mtu asiyekuwa kiakili, amekuwa ni mtu wa kupaniki sana anapokutana na jambo.

Ukiachana na kuwa mwanamitindo na Designer wa Wema kwa kipindi cha nyuma, Martin pia alishawai kuwa meneja wa Wema Sepetu lakini baadae walisitisha kazi hizo na sasa wamebaki kuwa marafiki tu.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.