Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Mimba Iliyotoka Na Muhusika Wa Mimba Hiyo

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka kuhusu janga lilompata hivi katibuni baada ya kuweka wazi kuwa mimba aliyokuwa amebeba kwa mara ya pili imetoka Tena.

Wema amekuwa muwazi sana juu ya kipindi kigumu  akijaribu kutafuta mtoto kwani sio mara ya kwanza kwa Wema kuweka wazi kuwa amepata miscarriage kwani miaka michache iliyopita mimba yake na Idris Sultan ilichoropoka.

download latest music    

Wiki iliyopita Wema Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka wazi machungu yake baada ya kuandika kuwa kwa mara ya pili mimba aliyokuwa amebeba imetoka tena.

Mara moja baada ya habari hizo kusambaaa tetesi nazo zilianza kutembea kuwa muhusika wa mimba hiyo hakuwa mwingine bali ni staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye alisemekana kuwa na Mahusiano naye.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Wema amekataa tetesi hizo na kudai Diamond hakuwa muhusika wa mimba hiyo kabisa na kumtaja mwanaume mwingine:

Hakuna ukweli wowote, ni ya mtu mwingine kabisa Diamond ni Hakuna lolote ila ni mshkaji wangu ambaye si unajua tumezoeana sana!”.

Lakini pia Wema aliweka wazi kuwa mimba yake iitoka muda mrefu uliopita ila aliweka wazi wiki iliyopita:

Kusema ukweli hiyo mimba imetoka karibia mwezi na nusu hivi umepita lakini kilichotokea Mimi niliweka picha moja ya mwanamke mwenye tatizo kama langu la kushika mimba kisha inatoka ndipo nikaandika; ‘My Life Story’.  

Hapo ndipo watu walichukulia kama nimepatwa na janga hilo kwa wakati huu, lakini ukweli ni jambo lililonipata mwezi na nusu uliopita“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.