Loading...

Wema Sepetu Agoma Kushiriki Katika Maombi

November 08, 2018 at 12:37
Wema Sepetu Agoma Kushiriki Katika Maombi

Kuna tangazo lilikuwa likipita katika mitandao ya kijmii likielezea na kutoa taarifa kuwa mwanadada Wema sepetu atakuwepokatika moja ya makongamano ya dini lililokuwa likitegemewa kufanyika wikiendi hii katika kanisa moja  jijin dar.

Baada ya kusambaa sana kwa taarifa hzio, mwanadada wma sepetu ameibuka na kukanusha taarifa hizo na kusema kuwa huo ni uongo kwa sababu hata tangazi hilo lilipotoka hakuna na taarifa nali lakini pia hawezi kufanya kitu kama hiko.

Loading...

Wema anasema kuwa hata yeye amekuwa na shida nyingi ikiwemo kilio chake cha kupata mtoto lakini hawezi kwenda katika  mkesha usiokuwa na taarifa rasmi.

Akikanusha taarifa hizo katika ukurasa wake wa instagram, wema anasema kuwa amechukizwa sana na uwepo wa taarifa hizo ambazo yeye hakuwa na habari nazo hata kidogo na wala hakutoa rughusa ya jambo hilo.

Wema anasma kuwa amekuwa akisikia kuwa kuna watu wanajikusanya kwa ajili ya kumfanyia maombi na aliona kuwa hayo ni mapenzi ya dhati lakini swala la yeye kuwepo katika mikesha mbalimbali kwa dhumuni hilo ambalo wanalisema kwake yeye hakuwa na hizo habari kabisa.Wema anasema kuwa ni kweli kwa sasa amekuwa mgonjwa lakini hakuna ukweli wa kuwepo katika mikesha hiyo.

 

Share

Comments

  1. Ni vizuri umeweka jambo hilo wazi

  2. Binadamu ni wanafiki sana

  3. Watu wasitumie jina la watu kujinufaisha bila ruhusa

  4. ? ?

  5. Na vile nilitaka kuja ili nikuone kumbe ni uwongo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…