Wewe Ulinibadilisha na Kunifanya Niache Kupiga Picha za Nusu Uchi -Maneno ya Gigy kwa Ruge

Moja ya wasanii ambao kwa sasa wamepata majina makubwa bongo kutokana na kazi zao, Gigy money amefunguka na kutoa maneno yake ya huzuni hasa baada ya kusikia kifo cha mkurugenzi wa Clouds media groud bwana Ruge Mutahaba.

Gigy money ameandika ujumbe mrefu na wenye kuhuzunisha akijitahidi kuonyesha mchango wa mkurugenzi huyo katika maisha yake huku akimwita kuwa yeye ndio mzazi wake baada ya mama yake aliemlea.

download latest music    

Gigy money anasema kuwa Ruge ndie aliemfungulia maisha kwa kumpa nafasi hata katika kituo chake kama mfanya kazi hapo huku akijitahidi kil siku kumyoosha katika njia mbaya alizokuwa akipita.

Gigy anasema kuwa hata ile tabia yake ya kupiga picha za uchi , ni Ruge ndie alimfanya kuachana na swala hilo kutokana na kuwa kila mara alikuwa akimjali na kuongea nae ili kujaribu kumbadilisha.

https://www.instagram.com/p/BuWuw-MntWs/

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.