Loading...

Wivu wa Mume wa Linah Wamkosesha Mikataba ya Kazi

March 13, 2018 at 09:21
Wivu wa Mume wa Linah Wamkosesha Mikataba ya Kazi

Mwanamuziki aliyekuwa anafanya kazi nchini Kenya, Mr. Kesho amefunguka na kudai kila wivu aliokuwa nao mume wa Linah ambaye pia ni meneja wake Shaban Mvhomvu unamkosesha mkataba wa kazi na Linah.

Mume wa Mwanamuziki wa Bongo fleva Linah Sanga ambaye pia ni mzazi mwenzake Shaban Mchovu maarufu kama Director Ghost amedaiwa kuwa na wivu sana kwa mkewe kiasi ya kwamba ameshindwa kupata kazi.

Loading...

Mr. kesho amefunguka kuwa aliporudi kufanya nchini Tanzania alianza kusimamiwa na Adam Mchomvu ambaye pia alikuwa anamsimamia Linah lakini baada ya kutoa wimbo mmoja aliondoka kwenye label hiyo na inasemekana kabisa kuwa chanzo ni ukaribu wake na Linah.

Ukaribu wake na Linah ulisababisha habari kuenea kuwa anatoka kimapenzi na Linah jambo ambalo linasemekana halikumfurahisha meneja ambaye ni mpenzi wa Linah.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Mr. Kesho amefungukia tuhuma hizo za kuwa na Linah na ukaribu wao:

Hapana hakuna kilichoendelea kati yangu mimi na Linah ila tu alikuwa ni mshkaji wangu ambaye nina nyimbo naye tumefanya naye wimbo hakuna mapenzi kati yangu na Linah lakini kama meneja alikataa kurenew mkataba kisa wivu basi sio kosa langu”.

 

Share

Comments

  1. wah

  2. hutendeka

  3. makosa sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…

wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.