Loading...

Wolper afungukia tetesi za yeye kutaka kumtolea mahari na kumuoa mpenzi wake

September 09, 2017 at 17:12
Wolper afungukia tetesi za yeye kutaka kumtolea mahari na kumuoa mpenzi wake

Baada ya tetesi kuenea mitandaoni kuwa Jackline Wolper anataka kumtolea mahari na kumuoa mpenzi wake “ben-ten”Brown ambaye ana umri mdogo kuliko yeye  Wolper ameibuka kupitia ukurasa wake wa instagram na kukana na kuzima habari hizo huku akidai kuwa yeye sio muhindi kwani wahindi wanawake ndo wanaoa wanaume.

Habari hizo zilienea baada ya gazeti la udaku kuripoti kuwa Wolper alidai wabongo wengi wamezoea kuona mwanaume ndiyo anatoa mahari na kuoa jambo ambalo kwake anaona ni utaratibu na uamuzi tu si dhambi mwanamke kumlipia mahari mwanaume. Wolper aliendelea kusema:

download latest music    

“Unajua watu wengi wanachukulia mahari ni lazima atoe mwanaume kitu ambacho siyo sahihi kabisa maana hata India siku zote  mwanamke ndiyo anatoa mahari na mimi nataka kuanzisha hiyo bongo. “Najua katika hili, watu wengi wataanza maneno maneno kuwa mimi ndo nimeoa lakini sitajali”.

Kupitia ukurasa wake wa instagram pamoja na kukana kuwa hataki kumuoa Brown kama magazeti ya udaku yalivyodai pia ametumia nafasi hiyo kuelezea hisia zake juu ya mpenzi wake huyo kuwa anampenda na na anapokuwa na yeye moyo wake unajawa na amani na furaha na kumuita mwana wa maisha yake.

Wolper alianza ku-date Brown miezi michache iliyopita baada ya kuachana na mpenzi wake wake wa siku nyingi mwanamuziki Harmonize.  Wolper na Brown walipata umaarufu mkubwa mtandaoni kutokana na umri mdogo wa Brown.

Loading…

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment