Loading...

Wolper Akacha Kumsapoti Harmonize Kikazi ili Kulinda Mahusiano yake na Sarah

April 16, 2018 at 14:33
Wolper Akacha Kumsapoti Harmonize Kikazi ili Kulinda Mahusiano yake na Sarah

Muigizaji na mjasiriamali Jackline Wolper amefunguka na kusema kuwa ili kulinda mahusiano yamsanii huyo basi ameamua kuacha kumsapoti Harmonize katika kazi zake za kimuziki kwa sababu inaoneana kama bado ana mapenzi na msanii huyo wakati yeye ni kama shabiki tu.

Wolper ambae hakuwahi kuonekana mwenye roho mbaya kila unapotoka wimbo mzuri wa Harmonize amekuwa akionekana kuimba na kucheza, amesema kuwa anapofanya hivyo inakuwa inaonekana kama vile bado ana hisia za kimapenzi na mwanamuziki huyo wakati yeye akishaacha amaecha.

Loading...

Haya yote yanatokea pale wiki iliyopita ambapo Sarah mpenzi wa Harmonize alipomtuhumu  wolper kuwa amekuwa akimtumia  sms mwanaume wake na kuwa anaona kama Wolper anamsumbua na kumtaka mpezni wake ambapo Jacky alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa inawezekana kuna watu wanatumiwa na mwanamke huyo ili kumchafua.

Akiongea na sam misago, wolper anasema “mimi sio mswahili na wala sina uswahili tulianza mapenzi kwa mimi kuwa nasapoti kazi zake,lakini sasa hivi naona nisikukwaze  na nisiharibu mahusiano yako naona bora niache sababu yule mwanamke wake  anahitaji sana kuhurumiwa.’

Wolper alisema pia kuwa pamoja na kwamba ameacha kusapoti kazi lakini pia ameona kuwa ni bora kuwablock wote wawili ili kupeusha shari na watu hawa.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…